loader
Picha

Simba yapotezwa Congo

SIMBA jana iliaga michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kukubali kipigo cha mabao 4-1 dhidi ya TP Mazembe ya Congo DR.

Wawakilishi hao wa Tanzania, walihitaji ushindi au sare yoyote ya mabao kusonga mbele baada ya kutoka suluhu nyumbani dhidi ya mabingwa hao wa zamani wa Afrika, lakini hali ilikuwa tofauti.

Mchezo huo wa robo fainali ulichezwa jana kwenye uwanja wa Mazembe mjini Lubumbashi na kwa ushindi huyo Mazembe imetinga nusu fainali za michuano hiyo. Mabao yalifungwa na Emmanuel Okwi kwa upande wa Simba na Mazembe ni Kabaso Chongo, Meshack Elia, Tresor Mputu na Jackon Muleka.

Simba ndio walitangulia kupata bao la uongozi dakika ya pili, likifungwa na Okwi baada ya kupata pasi ya kiungo Haruna Niyonzima. Mazembe walicharuka na kuanza kushambulia lango la wekundu hao na kusawazisha dakika ya 23 kupitia kwa Elia na baadaye dakika ya 38 Chongo akifunga la pili.

Mbali ya kuongoza, Mazembe pia ilitawala mchezo huo tangu walipoapata bao la kusawazisha mpaka mwisho wa mchezo.

Simba ilikianza kipindi cha pili kwa mabadiliko kwa kuwatoa Mzamiru Yassin na Juuko Murshid, Okwi na nafasi zao kuchukuliwa na Cletous Chama, Meddie Kagere na Rashid Juma.

Mabadiliko hayo hayakusaidia zaidi ya Mazembe kuongeza kasi ya kushambulia na kuongeza bao la tatu na la nne dakika ya 62 na 73 yakifungwa na Mputu na Muleka.

Mazembe walitengeneza nafasi nyingi za kufunga kama wangetulia walikuwa na uwezo wa kufunga mabao zaidi ya hayo.

Lakini pia, kwa upande wa Simba dakika za mwishoni walijaribu kushambulia na kutengeneza nafasi ila hazikuzaa matunda. Simba sasa inarudi nchini kuelekeza nguvu zake kwenye kutetea taji la Ligi Kuu ambapo ina viporo tisa

TIMU nne zinazopeperusha bendera ya nchi kimataifa kwenye Ligi ya ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi