loader
‘Wanaokwamisha miradi ya maendeleo kuhamishwa’

‘Wanaokwamisha miradi ya maendeleo kuhamishwa’

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewaweka kitimoto wakuu wa idara mbalimbali zilizopo katika halmashauri za wilaya na jiji hilo kwa kuwataka kujiandaa na uhamisho kwenda mikoani endapo idara zao zitabainika kukwamisha miradi mbalimbali.

Akizungumza katika kikao cha dharura cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Makonda alisema tayari ofisi yake imeanza kulifanyia kazi suala hilo ikishirikiana na Ofisi ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) kwa hatua hiyo. Kwa mujibu wa Makonda baadhi ya watendaji hao hususani waliokaa katika ajira zao ndani ya Jiji hilo kwa zaidi ya miaka 10 bila uhamisho wowote, wamekuwa kikwazo katika mikakati mbalimbali iliyo katika Mpango wa Maendeleo kutokana na mazoea waliyoyajenga na wadau mbalimbali wakiwemo wakandarasi.

“Baadhi yenu hapa wamekuwa wakikwamisha kwa makusudi miradi hiyo, wamekuwa wakiwakwamisha wakurugenzi, mameya, wakuu wa wilaya na hata mimi mkuu wa mkoa. Kifupi watambue kuwa mwisho wao ndani ya Jiji hili ni mwezi ujao,” alisema Makonda.

Aidha Makonda alimuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo ya Ilala, Jumanne Shauri kumsimamisha mmoja wa wakandarasi ambaye siku za hivi karibuni alilalamikiwa na mmoja wa madiwani wa halmashauri hiyo kwa kufanya kazi aliyopewa chini ya kiwango. “Nakutaka mkurugenzi kumsimamisha kazi mkandarasi huyo mara moja na kama wapo wengine wasimamishe hatuwezi kuona fedha zikipotea kwa kazi sizizo na ubora,” alisema Makonda.

Alisema wao kama viongozi vigezo vyao vya utendaji kazi vinapimwa kutokana na kazi wanazozifanya na kwamba hawapo tayari kuona wanapoteza kazi hizo kutokana na makosa yanayofanywa na watu wengine tena kwa kuzembea. Katika hatua nyingine, Makonda amedai kubaini matukio ya ubadhirifu wa fedha katika miradi ya ujenzi wa barabara inayotekelezwa kupitia Mpango wa Uendelezaji wa Miji (DMDP), suala alilolitaka baraza hilo kulifanyia kazi ili kujiridhisha nayo.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/8b68d65743b4d22318155fa3fa42ecda.jpg

WAFANYAKAZI wa Kituo cha Redio ...

foto
Mwandishi: Oscar Job

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi