loader
Picha

Akanusha fedha za TRA kutumiwa Bara

MAMLAKA ya Mapato Nchini (TRA) imesema fedha za kodi zinazokusanywa Zanzibar kutoka kwa wananchi na wafanyabiashara zinabakia visiwani kwa ajili ya shughuli za maendeleo.

Hayo yalisemwa na Ofisa kodi TRA, Omar Abdalla Kirobo katika mkutano na masheha na madiwani kuwaeleza umuhimu wa kulipa kodi huko visiwani Pemba. Alisema zipo dhana za baadhi ya watu ikiwemo wafanyabiashara kwamba fedha za kodi zinazokusanywa Zanzibar jioni hupelekwa Tanzania Bara kwa matumizi ya huko. “Si kweli fedha za kodi zinazokusanywa Zanzibar zinabakia hapa na kutumika kwa ajili ya shughuli za maendeleo kwa wananchi wa Unguja na Pemba,” alisema.

Kirobo alisema kwamba nchi haiwezi kupata maendeleo na kutekeleza miradi ya jamii kama wananchi na wafanyabiashara watashindwa kulipa kodi inayostahiki kwa mujibu wa sheria. Ofisa wa Elimu ya kodi na huduma kutoka TRA, Abdalla Seif aliwataka viongozi wa shehia ikiwemo masheha na madiwani kuhamasisha ulipaji wa kodi kwa hiari kwa ajili ya maendeleo ya taifa.

Baadhi ya madiwani na masheha waliitaka mamlaka kutoa elimu zaidi kuhusu umuhimu wa kulipa kodi ili jamii ifahamu malengo yake na fedha zinazokusanywa zinatumika kwa ajili ya kazi gani. “Tatizo moja kubwa jamii yetu haifahamu umuhimu wa kulipa kodi kwa maendeleo ya taifa, lakini na taasisi za mapato nazo zitoe elimu zaidi,” alisema Khatib Chwaya, sheha wa Wete Pemba.

MKUU wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi