loader
Picha

Marcelino aitisha Arsenal

KOCHA wa Valencia Marcelino amesisitiza presha itakuwa kwa Arsenal wakati kikosi chake kitakapowavaa washika bunduki hao kwenye mechi ya nusu fainali za michuano ya ligi ya Europa.

Toni Lato na Dani Parejo walikuwa nyota juiz kwa Los Che wakiifunga Villarreal mabao 2-0 na kuibuka na ushindi wa jumla ya mabao 5-1 na kufuzu nusu fainali. Marcelino hakufurahishwa sana na kikosi chake kilivyocheza kwenye mechi ya kwanza, lakini kilimshangaza kwa namna kilivyong’ara Mestalla. Kwenye mechi za nusu fainali wanakutana na Arsenal inayoongozwa na mshindi mara tatu wa ligi ya Europa na kocha wa zamani wa Valencia Unai Emery na Marcelino amesisitiza kwamba timu hiyo ya Ligi Kuu ndiyo inayopewa nafasi kubwa kushinda.

“Arsenal inapambana kupata tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa, ikiwa na kocha anayefahamu vizuri kuwa wanapewa nafasi kubwa,” alisema Marcelino kwenye mkutano na waandishi wa habari. “Lakini lolote linaweza kutokea kwenye nusu fainali, wakati huohuo kwenye fainali Baku. “ Valencia ilimaliza mwanzo mgumu wa kampeni hizi, lakini kikosi cha Marcelino kipo na tofauti ya pointi tatu kwenye nne bora za LaLiga, huku fainali za kombe la Copa del Rey dhidi ya Barcelona inawasubiri. “Tunajivunia kiwango kilichoonyeshwa na kikosi chetu, tupo kwenye nusu fainali na kisha fainali,” alisema Marcelino “Kushinda Seville [dhidi ya Real Betis Jumapili] kutatuweka kwenye hali nzuri.”

MCHEZAJI wa Barcelona, Philippe Coutinho, ametua Ujerumani kwa ajili ya ...

foto
Mwandishi: LONDON, England

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi