loader
Picha

Asilimia 73 ya miti iliyopandwa Lindi inaendelea kukua vizuri

MITI 4,170,076 sawa na asilimia 73.4 kati ya mti 5,356,887 iliyopandwa kati ya mwaka 2017 na 2018 mkoani Lindi imepona na kuendelea kukua.

Taarifa hiyo imetolewa na Ofi sa Maliasili na Mazingira wa Mkoa wa Lindi, Zawadi Jilala wakati wa maadhimisho ya siku ya upandaji miti kimkoa iliyofanyika wilayani Kilwa. Jilala alisema katika taarifa yake hiyo kwamba lengo la kupanda miti kwa miaka hiyo lilikuwa 7,500,000 hivyo miti iliyopandwa 5,356,887 ni na asilimia 71.3 ya lengo.

Katika hafla hiyo iliyofanyika shule ya sekondari ya kutwa ya Kilwa ambapo miti 600 ilipandwa katika uzinduzi huo, Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi aliwataka watendaji wakuu wote wa halmashauri sita za mkoa huo kuhakikisha kwamba shughuli ya upandaji miti ni endelevu na wala si la matukio.

Alisema Mkoa wa Lindi wenye jumla ya kilometa 67,855.32 sawa na hekta 6,785,532 ambazo kati ya hizo hekta 5,238,431 sawa na asilimia 77.2 ya eneo la mkoa zimefunikwa na uoto wa asili ambao ni misitu na mapori, ni lazima kukazana kupanda miti ili kuendelea kuwa na hali njema.

Zambi alisema mapinduzi ya viwanda yanawezekana kwa kuhifadhi mazingira na kuhakikisha uvunaji wake unakwenda kwa mujibu wa taratibu. “Ingawa mkoa una misitu isiyoingiliwa sana na kuharibiwa sana ukilinganisha na mikoa mingine, ipo haja ya kuhakikisha rasilimali hizi haziharibiwi,” alisema mkuu wa mkoa katika hotuba iliyosomwa na Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Christopher Ngubiagai.

Mkoa wa Lindi una msitu ya hifadhi isiyopungua hekta 829,510.5 ambayo imehifadhiwa kisheria. Miongoni ma misitu hiyo kuna msitu ya hifadhi ya taifa hekta 370,504, misitu ya hifadhi ya vijiji hekta 453,283.5;misitu ya mikoko hekta 44,038 na misitu ya kupandwa hekta 3,000. Misitu ya hifadhi ya vijiji mingi ipo katika Mradi wa usimamizi shirikishi wa misitu (PFM) ambao umewezeshwa na Shirika la kuendeleza na kuhifadhi Mpingo (MCDI) chini ya ufadhili wa WWF.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, Abuu Mjaka alisisitiza haja ya upandaji wa miti kuwa endelevu kwa kuwa kila kitu anachohitaji binadamu msingi wake mkubwa ni miti na misitu. Mtendaji wa zamani wa misitu na Mwenyekiti wa bodi ya MCDI, Dk Felician Kilahama aliwataka wanamuziki kuhamasisha upandaji wa miti kupitia muziki ambao upo katika kila basi la abiria. Aidha Kaimu katibu tawala mkoa wa Lindi Dk Bora Haule alitaka kuwepo na kanzidata ya miti iliyopandwa na kupona.

MTENDAJI wa Kijiji cha Manchali A, Wilaya ya Chamwino mkoani ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Kilwa

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi