loader
Picha

TPA sasa yafanya kazi saa 24 siku zote 7

MAMLAKA ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), imesema utendaji kazi wa bandari, unaendelea kuboreka zaidi kwa kuwa na shehena kubwa bandarini na kufanya kazi saa 24 kwa siku na siku zote saba za wiki.

Kwamba kwa mwezi Machi mwaka huu wamehudumia meli 22 ukilinganisha na meli kati ya 10 hadi 15 za awali. Sambamba na hilo, TPA imesema idadi ya shehena za magari zinazoingia bandarini hapo, inaongezeka kama ilivyokuwa hapo awali ya magari 180,000 mwaka 2013/14, kabla ya kuporomoka hadi 47,000 mwaka 2017/18 na sasa wanategemea kupokea magari 200,000 kwa mwaka 2018/19.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuhusu utendaji kazi wa TPA kwa jumla na wakati huu wa sikukuu za Pasaka,Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Deusdedit Kakoko alisema ongezeko hilo la shehena linatokana na kuboreka kwa utendaji kazi wa mamlaka. Alisema hivi sasa wanafanya kazi saa 24 kwa siku na siku zote saba za wiki na kwamba wadau wengine wa bandari nao wanafanya vivyo hivyo. Kwamba wale wasiofanya wanapaswa kuwajibishwa kwa sababu walishapewa utaratibu wa kufanya kazi kwenye sekta hiyo.

“Bandari inafanya kazi saa 24 na siku saba na pia msimu huu wa sikukuu tuko kazini kama kawaida, lakini wakati mwingine mfano sikukuu hizi zinazofuatana baadhi yetu hawafanyi kazi kikamilifu ila sisi tumeitana na kuimarisha hali ya usalama bandarini,” alisema. Aliongeza kuwa, “taasisi nyingine za serikali zaidi ya 34 bandarini wote tuhakikishe tuko kazini saa 24 tupange maofisa wetu muda wote, ili kazi ziendelee kufanywa za kutoa mizigo na za ulinzi viende kwa utaratibu uliowekwa.” Akizungumzia kuongezeka kwa shehena bandarini, Kakoko alisema bandari imeendelea kupata mzigo wa kutosha.

Alisema mwezi uliopita walianza kuhudumia meli kati ya 10 hadi 15 na kisha ziliongezeka hadi kufikia meli 22, kiwango ambacho ni kikubwa. Alisema baada ya kuongezeka kwa idadi hizo za meli. walianza kutumia gati jipya namba moja ambalo ni sehemu ya mradi wa maboresho ya bandari ya Dar es Salaam yenye urefu wa mita 15.5 na ndio gati refu kuliko yote na linaweza kutokea meli ya ukubwa wowote kwa sasa.

“Baada ya meli kuongezeka bandarini, ilibidi tuchukue hatua ya kutumia gati jipya namba lenye urefu wa mita 15.5 ndio gati refu kuliko zote na meli kubwa iliyobeba shehena ya vifaa vya mradi wa Kinyerezi 11, ndio ilianza kuitumia gati hilo wakati huo lilikuwa bado hakijakamilika vizuri, ila sasa liko tayari,”alisema Kakoko. Sambamba na kuanza kutumia gati hilo, pia nafasi bandarini ya kuweka mizigo nayo ilipungua na waliomba eneo la Ticts, ila nao walikuwa na sehena nyingi, ndipo wakatumia eneo jingine la bandari lililo ndani ya bandari, ambalo lilikuwa halitumiki miaka mingi. “Eneo hilo lipo karibu na makutano ya Reli ya Kati na ile ya Tanzania na Zambia, panaitwa Kitopeni, ni eneo la yadi kwa ajili ya kuweka magari”,aliongeza Kakoko.

MTENDAJI wa Kijiji cha Manchali A, Wilaya ya Chamwino mkoani ...

foto
Mwandishi: Ikunda Erick

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi