loader
Picha

Tamisemi watoa mil 513/- kujenga madarasa 41

MKUU wa Wilaya ya Lushoto, January Lugangika amesema kuwa Wizara ya Nchi, Ofi si ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) imetoa kiasi cha Sh milioni 513 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba 41 vya madarasa.

Akizungumza na gazeti hili Mkuu huyo wa wilaya hiyo alisema kuwa fedha hizo zimeletwa Machi 26, mwaka huu.

Alifafanua kuwa kabla ya fedha hizo kutolewa tayari wananchi wamejenga vyumba hivyo vya madarasa hadi kufikia hatua ya linta kilichobaki ni kuezeka ambapo ujio wa fedha hizo utafanikisha kukamilisha ujenzi wa vyumba hivyo.

“Wilaya ya Lushoto ina upungufu wa madarasa 41 ambapo jumla ya wanafunzi 1,300 walikuwa wamezidi kutokana na uwiano wa wanafunzi arobaini kwa darasa, ili kuhakikisha wanafunzi wote wanasoma tuliwaweka kwenye vyumba vya sasa na kufanya darasa kuwa na wanafunzi hamsini,” alisema.

Aliongeza kuwa hadi kufikia mwisho wa mwezi Aprili watakuwa wamekamilisha ujenzi wa vyumba hivyo baada ya ujio wa fedha hizo. Katika hatua nyingine mkuu huyo wa wilaya alisema wilaya hiyo imeweka mikakati ya kuhakikisha wanafunzi wote wa kidato cha sita wanaotarajiwa kufanya mtihani wa Taifa Mei 6, mwaka huu wanafaulu katika daraja la kwanza na kujiunga Chuo Kikuu.

Alitaja mikakati hiyo kuwa ni kuhakikisha kila mwanafunzi anayepata daraja la kwanza anapewa zawadi ya Sh 300,000, mwalimu atayefaulisha masomo ya tahasusi (combination) naye anazawadiwa kiasi cha Sh 300,000, shule itakayofanya vizuri itapewa 500,000 na mwanafunzi anayeingia hatua ya kumi bora atazawadia kiasi cha Sh 200,000.

Wilaya ya Lushoto ina jumla ya shule kumi za kidato cha tano na sita za binafsi na za serikali zikiwemo shule zinazoongoza ikiwemo Kifungilo, Lwandai na Mazinde Juu.

MTENDAJI wa Kijiji cha Manchali A, Wilaya ya Chamwino mkoani ...

foto
Mwandishi: Cheji Bakari, Lushoto

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi