loader
Picha

Mavunde: Someni mje mzibe pengo

WANAFUNZI wa kidato cha sita waliopo kambi maalum ya kitaluma, wametakiwa kuepuka makundi, ngono zembe, na matumizi ya dawa za kulevya na badala yake wasome kwa bidii na kuziba pengo la watu wasiokua na ujunzi ifikapo 2025.

Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira, na Watu wenye ulemavu, Anthony Mavunde alipotembelea kambi hiyo iliyopo Shule ya Sekondari ya Maswa mkoani Simiyu.

Mavunde alisema kuwa Tanzania Ina upungufu wa watu wenye ujuzi na kwamba kati ya watanzania milioni 57, kati yao milioni 22.3 wenye uwezo wa kufanya kazi, asilimia 3.6 pekee ndio wanaujuzi wa just, huku asilimia 16.5 wanaujuzi wa kati na asilimia 79.9 Wana ujuzi wa chini zaidi.

Alisema iwapo wenye ujunzi mkubwa hawataongezeka, malengo ya serikalo kufikia uchumi wa kati itakua ndoto.

"Ili kufikia lengo la uchumi wa kati ni laza watu wenye ujuzi kuongezeka, asilimia 12 wenye ujuzi wa juu, ujunzi wa kati asilimia 34 na ujunzi wa chini kabisa asilimia 54,"alisema.

Mavunde aliwataka wanafunzi hao kusoma kwa bidii ili wazibe pengo lililopo na kuleta ushindani katika soko la ajira la sivyo watakua na safari ndefu kimaisha.

"Vijana mnaosoma mna kazi kubwa sana,mnatakiwa kusoma kwa bidii ili muwe Bora katika soko la ushindani, Kama unamua kuwa injia basi uwe bora, Kama daktari uwe bora zaidi, hali kadhalika kwenye fani nyingine." alisema.

Kwa upande wa mkuu wa mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka alisema kambi hiyo rasmi ya kitaaluma kwa Wanafunzi wa Kidato cha sita kwa mwaka 2019 ina wanafunzi 1166 na kuagiza taa zisizimwe usiku ili wanafunzi waweze kupata nafasi ya kujisomea zaidi.

Mtaka alisema pia Kuna jumla ya walimu mahiri 34 kutoka shule 12 za mkoa wa Simiyu, na imekua ni utaratibu kwa madarasa yenye mitihani kuwekwa kwenye kambi maalum, na walimu kuwafundisha kwa karibu na kuwapa mbinu mbali mbali za kujifunza.

Amesema ili mkoa wa Simiyu uweze kushindana kiuchumi unapaswa kufanya mageuzi makubwa ya kielimu, hivyo elimu ni kiupaumbele cha mkoa ambapo ameagiza katika kipindi chote cha kambi wanafunzi waruhusiwe kusoma bila kuzimiwa taa darasani.

MTENDAJI wa Kijiji cha Manchali A, Wilaya ya Chamwino mkoani ...

foto
Mwandishi: Vicky Kimaro

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi