loader
Picha

TBS yateketeza tani 3 ya nguo za ndani

SHIRIKA la Viwango nchini (TBS) limeteketeza tani tatu za nguo za ndani za mitumba katika mikoa ya Mwanza na Mara.

Akizungumza jijini hapa jana Ofisa Ukaguzi kutoka TBS makao makuu Baraka Majige alisema nguo hizo zimebainika wakati wa ukaguzi ubora wa bidhaa linaloendelea kwa nchi nzima likitekelezwa na shirika hilo. “Tumeteketeza nguo hizo kwa mujibu wa kiwango cha ISO cha 758.17 kinachokataza matumizi ya nguo za ndani zilizokwishatumika kuuzwa kwa watu wengine na ambazo hazina ubora unaotakiwa kiafya,” alifafanua.

Akitoa ufafanuzi juu ya malalamiko ya wafanyabiashara wadogo maarufu kama machinga alisema kwamba iwapo watanunua bidhaa za nguo kutoka kwa wafanyabiashara wanaouza jumla na wakagundua zipo bidhaa za nguo zilizopigwa marufuku, watoe taarifa kwenye mamlaka za serikali ikiwemo TBS na polisi ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa mara moja.

“Mfanyabiashara wa jumla wa nguo za mitumba, atakayebainika kukiuka utaratibu huu uliowekwa na serikali atachukuliwa hatua zitakazomsababisha kujutia kosa lake, hakutakuwa na huruma,”alisema.

Kwa upande wake Ofisa Masoko wa TBS kutoka makao makuu Debora Haule alisema kuwa nguo hizo zilizotumika hususani nguo za ndani kama sidiria, nguo za ndani, taulo na leso ni rahisi kusambaza maradhi ya kuambukiza hasa saratani ya ngozi na magonjwa mengine ya zinaa, hivyo aliwataka wananchi waliozoea kutumia nguo hizo kwa matumizi ya kawaida kuachana na tabia hiyo kwani ni hatari kwa afya zao.

MTENDAJI wa Kijiji cha Manchali A, Wilaya ya Chamwino mkoani ...

foto
Mwandishi: Nashon Kennedy, Mwanza

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi