loader
Picha

Kidato cha 6 wapewa mbinu ya kufaulu

WANAFUNZI wa kidato cha sita waliopo katika kambi maalum ya kitaluma, wametakiwa kuepuka makundi, ngono na matumizi ya dawa za kulevya na badala yake wasome kwa bidii na kuziba pengo la watu wasiokua na ujuzi ifikapo 2025.

Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na watu wenye ulemavu, Anthony Mavunde alipotembelea kambi hiyo iliyopo Shule ya Sekondari ya Maswa mkoani Simiyu.

Mavunde alisema kuwa Tanzania ina upungufu wa watu wenye ujuzi na kwamba kati ya Watanzania milioni 57, milioni 22.3 wenye uwezo wa kufanya kazi, asilimia 3.6 pekee ndio wenye ujuzi huku asilimia 16.5 wakiwa na ujuzi wa kati na asilimia 79.9 wana ujuzi wa chini zaidi.

"Ili kufikia lengo la uchumi wa kati ni lazima watu wenye ujuzi kuongezeka, asilimia 12 wenye ujuzi wa juu, ujuzi wa kati asilimia 34 na ujuzi wa chini kabisa asilimia 54," alisema Mavunde aliwataka wanafunzi hao kusoma kwa bidii ili wazibe pengo lililopo na kuleta ushindani katika soko la ajira la sivyo watakua na safari ndefu kimaisha.

Kwa upande wa mkuu wa mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka alisema kambi hiyo rasmi ya kitaaluma kwa Wanafunzi wa kidato cha sita kwa mwaka 2019 ina wanafunzi 1,166 na kuagiza taa zisizimwe usiku ili wanafunzi waweze kupata nafasi ya kujisomea zaidi.

Mtaka alisema pia kuna jumla ya walimu mahiri 34 kutoka shule 12 za mkoa wa Simiyu na imekua ni utaratibu kwa madarasa yenye mitihani kuwekwa kwenye kambi maalum na walimu kuwafundisha kwa karibu na kuwapa mbinu mbali mbali za kujifunza.

Amesema ili mkoa wa Simiyu uweze kushindana kiuchumi unapaswa kufanya mageuzi makubwa ya kielimu, hivyo elimu ni kipaumbele cha mkoa ambapo ameagiza katika kipindi chote cha kambi wanafunzi waruhusiwe kusoma bila kuzimiwa taa darasani.

MKUU wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk ...

foto
Mwandishi: Vicky Kimaro

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi