loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

JOYCE SHEBE- Ruge, Kusaga wamenifikisha hapa

UNAPOZUNGUMZIA fursa zinazohusu maendeleo ya waandishi wanawake nchini na mambo mengine mengi yanayohusu utetezi wa haki ya mwanamke na mtoto wa kike ndipo unapokutana na chombo kijulikanacho kama Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA).

Tangu kuanzishwa kwa chama hicho ambacho miongoni mwa malengo yake ni kusimamia haki za wanawake na masuala mengine mbalimbali ya kijinsia, kimepitia katika uongozi wa viongozi mbalimbali.

Sasa kipo mikononi mwa Joyce Shebe, Mwenyekiti wa bodi aliyechaguliwa Aprili 5, mwaka huu.

Kabla ya Joyce,Tamwa imepita katika mikono ya wenyeviti takribani watano ambao ni Fatma Aluu, Edda Sanga, Ichikaeli Maro, Rose Ruben na Alakoki Mayombo aliyekabidhi kijiti kwa Joyce. Joyce anaamini kuwa Tamwa ni mali ya ambao kimsingi ndiyo wenye jukumu la kukijenga chama hicho.

Uchaguzi huo mbali na Shebe pia Tamwa iliutumia kuwapata wajumbe wa bodi hiyo ambao ni wanahabari Leah Mushi, Raziah Mwawanga na Halima Muselem kutoka Zanzibar ambao kimsingi wote kwa pamoja watahudumu katika nafasi zao kwa kipindi cha miaka mitatu.

Mwenyekiti huyo mpya ambaye pia ni Mhariri Mkuu wa kituo cha habari cha Clouds Media Group (CMG) inayohusisha vituo vya Redio na Televisheni, historia yake imepita katika maeneo mbalimbali lakini zaidi akiitumikia taaluma ya uandishi wa habari akiwa amebeba uzoefu wa zaidi ya miaka 18, akifanya kazi ndani ya taasisi mbalimbali zinazojishughulisha na masuala ya uhabarishaji.

Joyce ni mama wa watoto wawili, msomi wa Shahada ya Mawasiliano ya Umma, mbali na nafasi hiyo ya sasa pia anahudumu katika nafasi mbalimbali zilizopo ndani ya taaluma ya uandishi wa habari nchini kwanza kama mjumbe katika Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF).

Pia ni mjumbe katika Chama cha Wanahabari Dar es Salaam, Jukwaa la Wahariri juu ya Haki za Watoto (ECGCR) .

Akizungumzia kuchaguliwa kwake, Shebe anasema kilichomshawishi kutafuta uongozi ndani ya Tamwa ni nia yake ya kupenda mabadiliko mbalimbali yanayolenga ubunifu wenye tija kwa mandeleo ya chama hicho, wanawake, watoto na masuala mazima yahusuyo jinsia.

“Mimi si mzungumzaji sana, mimi ni msikilizaji zaidi. Lakini ninachoweza kusema kwa sasa ni kuwa Tamwa ni mali ya wanachama wote, sisi wanachama ndiyo tutakaoijenga Tamwa kutoka mahali ilipo sasa na kuipeleka mbele, zaidi ikijawa ubunifu utakaoiwezesha kupiga hatua,” anasema Joyce .

Anasema ili kufikia malengo hayo, wanawake wote hususani wanahabari wenzake kutumia kalamu zao vizuri kutoa ushirikiano kwa kuwa kufanya hivyo kwa kiasi kikubwa kutaweza kuibadili jamii na kuleta maendeleo ya taifa.

“Kupitia nafasi hii nimekusudia kujenga jamii itakayozingatia usawa wa kijinsia ambapo haki za wanawake na watoto zitaheshimiwa kama unavyofahamu Tanzania inakua nami kama Mwenyekiti mpya nitasimama katika kuhakikisha nasimamia mipango iliyokuwepo na mingine itakayokuja,”anasema Joyce.

“Niliingia kuomba nafasi hii nikiamini kuwa naweza kuipeleka Tamwa mbele, hiki kizazi kinachochipukia, niliamini naweza kusimama na kuitendea haki kama unavyoona tangu Tamwa imeanzishwa imepita kwa viongozi na kama utangaalia zaidi majukumu ya hiki chama siyo ya kukumbatiwa na mtu mmoja na ndiyo maana unaona viongozi wengi walipita na kufanya mambo mazuri hadi nipoingia” anasema Joyce, mtaalam wa habari za jinsia na maendeleo.

Anasema wakati anaingia kugombea nafasi hiyo, aliamini katika dhana ya ubunifu akibeba dhana ambayo kituo chake cha Clouds imekuwa ikiitumia hivyo kwa misingi hiyo akiamini uzoefu alionao utasaidia kuipeleka Tamwa ili iweze kufikia malengo yake ya kimaendeleo akiwa kama kijana anayejiamini katika nyanja mbalimbali zikiwemo za uongozi.

“Nimekulia Clouds nikiwa tangu binti mdogo, kama unavyotambua siku zote Clouds imekuwa njia kwa vijana wengi wenye malengo ya kupiga hatua kimaendeleo, naamini kuitendea haki nafasi hiyo kutokana na uzoefu nilionao na zaidi moyo niliojengewe na viongozi wangu wa hapa Clouds akiwemo Marehemu Ruge Mutahaba (Mungu amrehemu) pamoja na Mkurugenzi wa CMG Joseph Kusaga ambao kwa pamoja siku zote wamekuwa wakitutaka tuwe na ndoto kubwa,maeneo ambayo leo hii nakiri kuwa ndiyo yaliyonisukuma kufika hapa,” anasema Joyce.

Anasema mipango yake ndani ya chama hicho ni kuleta mabadiliko chanya yatakayoendana na mambo mengi yanayofanyika miaka ya sasa ikiwemo kupambana na ndoa pamoja na mimba za utotoni kiubunifu lakini pia kuwasimamia wanawake wote nchini ili waweze kuishi kiustawi na kuwawezesha kutimiza ndoto zao mbalimbali za kimaisha.

Anasema mikakati yake mingine ni pamoja na kukijenga chama hicho kwa kukifanya kuwa na nguvu za kifedha kupitia kwa rasilimali watu wake ambao kimsingi ni wanachama ambao mbali na kuwa wanahabari pia wana taaluma mbalimbali na hivyo kukiepusha chama kuwa ombaomba hata katika utatuzi wa changamoto wanazoweza kuzitatua wao wenyewe.

“Wakati nafikiria kugombea nilikua naiona tamwa kama chombo kinachohitaji ubunifu, hatua iliyonifanya nijione kwa nafasi yangu kama kuna kitu kinachonihitaji niwepo katika nafasi hiyo ili niwezekushirikiana na wanataaluma wenzangu ndani ya chama tuweze kuyafikia malengo ya kuanzishwa kwa Tamwa, nikiamini kwa fursa hiyo tunao uwezo wa kutosha kutimiza matakwa yetu,” anasema Joyce.

Anasema mikakati mingine ni kuongeza idadi ya wanachama ndani ya Tamwa ambayo tangu kuanzishwa kwake hadi sasa kimefikisha wajumbe 116, idadi aliyodai kuwa ni ndogo kiasi cha kukifanya chma kishindwe kufikia malengo yake kwa wakati kutokana na kukosa nguvu ya watu wengi kwa ajili ya kutoa mawazo na michango.

“Ili taasisi yoyote iwe na nguvu inapaswa kuwa na idadi kubwa ya wanachama ambao kwa nafasi zao wataweza kuisaidia kusonga mbele, hivyo naamini hata Tamwa endapo itaongeza wanachama hao itaweza kuwa mfano dhidi ya vyama na taasisi zingine mbalimbali, kikubwa ni nazidi kuwaomba waandishi kujitokeza na kujiunga ndani ya chama hiki kilichoanzishwa kwa ajili ya kushugulikia masuala yanayowahusu,” anasema Joyce.

Anasema kikubwa anachoomba ni ushirikiano kutoka kwa wanachama wenzake na waandishi wote wa habari ili kusaidiana kusukuma mbele malengo ya chama hicho na maendeleo ya Taifa kwa ujumla katika masuala mbalimbali ili kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais John Magufuli.

Anasema kupitia nafasi hiyo ya unyekiti anajiona kama kabeba mtu aliyebeba dhamana kubwa kwa wanahabari wote hususani wanawake wenzake suala linalomfanya ajione kama mtu mwenye deni kubwa dhidi yao ambalo kulilipa hakuna njia nyingine zaidi ya kujitoa kwa nguvu zake zote katika kuwatumikia

MIONGONI mwa vitu vinavyoweza kututofautisha binadamu ni namna tunavyopokea changamoto ...

foto
Mwandishi: Oscar Job

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi