loader
Dilunga aeleza siri ya ushindi Simba

Dilunga aeleza siri ya ushindi Simba

MSHAMBULIAJI wa Simba, Hassan Dilunga (pichani) ambaye alifunga bao pekee la ushindi juzi kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya JKT Tanzania amesema walicheza kwa kushambulia muda wote wakijua watapata nafasi adimu.

Alisema upana wa kikosi unawasaidia kushinda kila mechi na hata mchezo wa juzi uliochezwa Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, ambao walishinda 1-0. “Tulicheza vizuri ndio maana tulishinda, kuumia kwa John Bocco halikuwa pengo kwetu kwani sasa hivi kila mchezaji yupo vizuri na tuna kikosi kipana kila mchezaji akipata nafasi anaonesha kiwango,” alisema Dilunga.

Dilunga aliingia kipindi cha kwanza kuchukua nafasi ya John Bocco ambaye kocha Patrick Aussems alimtoa kwa sababu za kiufundi, kwani wana michezo mingi na hawana muda wa kupumzika kwa saa 72 kama kanuni zinazotaka. Simba imefikisha pointi 72 ikiwa katika nafasi ya pili nyuma ya Yanga yenye pointi 77 kileleni.

Simba itasafiri kwenda Mbeya ambako itacheza michezo miwili dhidi ya Mbeya City pamoja na Tanzania Prisons kesho na Mei 5 kabla ya kurejea Dar es Salaam kuendelea na mbio zake. Aidha kocha wa timu hiyo, Patrick Aussems amewapongeza wachezaji wake kwa kupambana hadi mwisho na kufanikiwa kupata pointi tatu muhimu zinazoendelea kuwaweka sawa kwenye mbio za ubingwa.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/8173c3794b1e93ebb1faeb71f8381167.jpeg

TAMASHA la muziki wa dansi ...

foto
Mwandishi: Rahel Pallangyo

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi