loader
Dstv Habarileo  Mobile
Kocha wa Man City amkubali Kompany

Kocha wa Man City amkubali Kompany

KOCHA wa Manchester City Pep Guardiola amekiri kumwambia Vincent Kompany asipige shuti katika ushindi dhidi ya Leicester juzi. Nahodha huyo wa City alifunga bao na kuipa timu yake ushindi wa 1-0 na hivyo kuifanya iwe na matumaini ya kutetea taji lake la Ligi Kuu kama itaifunga Brighton Jumapili.

Bao la juzi lilikuwa la kwanza nje ya eneo la hatari kwa beki huyo wa Ubelgiji Kompany baada ya miaka 11 akiwa na City. “Nilimwambia ‘usipige shuti Vinnie, usipige shuti,’’ alisema Guardiola.

Na Kompany alibainisha kuwa bosi huyo wa City hakuwa peke yake aliyeonyesha mashaka kabla hajapiga mpira huo. “Nilisikia watu wakisema ‘usishuti, usishuti’ lakini katika maisha yangu ya soka sikuwa na wachezaji chipukizi wakaniambia nisipige shuti,” alisema Kompany. Winga wa Manchester City Raheem Sterling aliweka picha ya Kompany akipiga shuti kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter na kuandika: “Uso wangu ulisawajika ‘hapana Vinny kwanini umefanya hivi’ ngumu, shuti kali, nahodha makini.” Kompany hajawahi kufunga kwa shuti nje ya eneo la hatari tangu mwaka 2013. Alifunga bao muhimu dhidi ya Manchester United mwaka 2012 na kurejesha matumaini ya kuwania taji.

Kompany amecheza mechi 16 za Ligi Kuu msimu huu na City imeshinda 15 kati ya hizo. Ameanza katika mechi tatu zilizopita dhidi ya Manchester United, Burnley na Leicester. Guardiola alisema amepanga kuzungumza na beki huyo kuhusu hatima yake mwishoni mwa msimu, huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 mkataba wake ukitarajiwa kufika mwisho. “Tutakunywa bia pamoja na kuamua kilicho bora, hasa kwa klabu,” alisema. “Ni mtu makini na ananisaidia sana, mara zote nasena sitamtumia sana lakini klabu hii iko kama ilivyo kwasababu watu wanampenda Vincent. “Anapokuwa fiti anakuwa makini kwenye nafasi ya beki wa kati, ni beki halisi, ni kiongozi mara nyingi.”

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/f919f0c35120cb3cdc56368c32c93a63.jpg

Kiungo mshambuliaji wa Brazil, Neymar JR amesema Kombe ...

foto
Mwandishi: MANCHESTER, England

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi