loader
Waziri mkuu Uingereza kujiuzulu Juni 7

Waziri mkuu Uingereza kujiuzulu Juni 7

WAZIRI Mkuu wa Uingereza, Theresa May (pichani) ametangaza kujiuzulu kama kiongozi wa Chama cha Conservative Juni 7 mwaka huu na kutoa fursa kuidhinishwa mchakato wa kuchaguliwa waziri mkuu mpya.

Katika taarifa aliyoitoa Downing Street, May amesema amefanya kila awezalo kutekeleza matokeo ya kura ya maoni kuhusu Umoja wa Ulaya(EU) ya mwaka 2016. May alisema ameshindwa kutimiza Mpango wa Kujitoa kwenye EU(Brexit) hivyo itaendelea kuwa ni jambo la majuto kwake. May amesema ataendelea kukaa kwenye nafasi ya waziri mkuu wakati kukitarajiwa kuidhinishwa mchakato wa kumchagua kiongozi mpya wa chama cha Conservative.

Atajiuzulu kama kiongozi wa chama hicho Juni 7 mwaka huu na uteuzi wa waziri mkuu mpya unatarajiwa kuanza wiki inayoafuata baada ya hatua hiyo. “Muda mfupi ujao nitaondoka kwenye nafasi hii ambayo imenipa heshima kubwa kuitumikia,”alisema May. May amesema mrithi wake atatakiwa kufanikisha muafaka wa pamoja kwa wabunge wote. May ambaye ni Waziri Mkuu wa pili mwanamke, amekaa kwenye nafasi hiyo kwa miaka mitatu.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/844738a8b96de5e548499880a2d6f0dd.jpg

MWENGE wa Uhuru unaendelea ...

foto
Mwandishi: LONDON, Uingereza

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi