loader
Simba kukabidhiwa kombe kesho

Simba kukabidhiwa kombe kesho

NAHODHA wa timu ya Simba, John Bocco amewaomba mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi kukisapoti kikosi hicho katika mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mtibwa Sugar kesho mjini Morogoro.

Mchezo huo pia utatumika kuwakabidhi Simba taji lao la ubingwa, baada ya Jumamosi kushindwa kukabidhiwa katika mchezo wao dhidi ya Biashara ya Mara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Bodi ya Ligi, Simba ilishindwa kukabidhiwa kombe hilo baada ya aliyetakiwa kuwa mgemi rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola kushindwa kutokea kwa sababu mbalimbali.

Mchezo huo wa 38 wa kufunga pazia kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara unatarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Jamhuri Morogoro, ambako pia watakabidhiwa Kombe la Ligi Kuu, ambalo wamelitwaa kwa mara ya 20.

Katika mchezo huo wa juzi, Simba walilazimishwa sare ya kufungana 1-1 na Biashara.

Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura amethibitisha kuwa Simba sasa watakabidhiwa Kombe Jumanne katika mchezo wake dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Jamhuri.

Bocco alitoa kauli hiyo baada ya kukamilika mchezo wa juzi dhidi ya Biashara akiwasisitizia mashabiki wao kujitokeza kwa wingi mjini Morogoro kuwashangilia katika mchezo huo na kusherehekea taji hilo, ambalo wamelitwaa mara mbili mfululizo.

“Kwa kutambua mchango wa mashabiki wetu ambao wanatuunga mkono kwenye michezo mingi na wamekuwa chachu ya kupata ushindi nawaomba wajitokeze kwenye mechi hiyo ili tupate ushindi utakaopamba taji letu,” alisema Bocco.

Aidha, Bocco amewaambia wanachama wa timu hiyo kilichosababisha washindwe kupata matokeo ya pointi tatu muhimu kwenye mchezo juzi ni mazingira ya uwanja kujaa maji.

“Hali iliyotufanya kushindwa kumiliki mpira kama iliyozoeleka kwenye mfumo wa uchezaji wetu wa kila siku, lakini hayo ni matokeo ya mpira hakuna namna tumeyapokea ingawa haukuwa mpango wetu kama timu,” alisema Bocco.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/77b051dca2fa65c692b708fc7d0c5633.jpg

TAASISI ya Mama Ongea ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi