loader
Dar mwenyeji mkutano wa SADC Agosti

Dar mwenyeji mkutano wa SADC Agosti

JIJI la Dar es Salaam linategemea kupokea wageni wengi wakiwemo marais, Agosti mwaka huu watakaokuja kushiriki mkutano wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

Kwa ugeni huo, wakazi wa jiji hilo wanaaswa kuliweka jiji katika hali ya usafi kuanzia utekelezaji wa katazo la matumizi ya mifuko ya plastiki nchini. Mkuu wa mkoa huo, Paul Makonda alisema hayo jijini Dar es Salaam na kuvitaka vikosi kazi vinavyosimamia agizo la katazo la mifuko ya plastiki kutumia muda huu kuhakikisha wanaliweka jiji katika mazingira safi na yenye kuvutia ugeni huo.

“Jiji linahitaji kuendelea kuwa safi, barabara inayotoka uwanja wa ndege itaboreshwa ifanane na ya kimataifa,” alisema Makonda na kuiomba Wizara ya Maliasili na Utalii kuweka matangazo ya kitalii katika barabara hususani inayotokea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) ili kuitumia fursa hiyo kwa kujitangaza kitalii.

Kadhalika aliwataka wakazi wa jiji hilo kutumia fursa ya mkutano huo na kunufaika kiuchumi, lakini pia wakiunganisha nguvu ili kuboresha mazingira. “Mara zote kunapokuwa na ugeni kama huo ni vyema wakazi wakachangamkia fursa mbalimbali zinazoweza kujitokeza, maana ni ugeni mkubwa ambao unaweza kuleta chachu ya kuongeza uchumi au kipato kwa wananchi,” alisema Makonda.

Alisema Rais John Magufuli anatarajiwa kuongoza mkutano huo, hivyo vikosi kazi vyote vinavyosimamia suala la kuzuia matumizi ya mifuko ya plastiki, kusimamia kwa hali wakizingatia kutoa elimu zaidi ili wananchi na takataka kupelekwa katika vituo vinavyotakiwa.

Alisema mji unatakiwa kuendelea kubaki kuwa msafi, kuanzia katika barabara ikiwemo ile inayotoka uwanja wa ndege ambayo itaboreshwa pamoja na barabara nyingine. Makonda alisema kupitia mkutano huo wananchi waunganishe nguvu ili kuboresha pia mazingira, huku akiamini kuwa suala la usafi litafanywa vizuri.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/48aba817d69bdc8ea78d42878d5d609b.jpg

WAFANYAKAZI wa Kituo cha Redio ...

foto
Mwandishi: Lucy Lyatuu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi