loader
Simba, Yanga zamsaka mchezaji Harambee Stars

Simba, Yanga zamsaka mchezaji Harambee Stars

WINGA nyota wa timu ya Bandari na timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars, Abdallah Hassan amethibitisha kufuatwa na vigogo vya soka vya Tanzania, Simba na Yanga vikitaka kumsajili.

Hata hivyo, Hassan hajasema kama yuko tayari kwenda kucheza soka katika timu ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara. Alisema ni jambo la kawaida kwa klabu kujaribu kumchukua mchezaji katika kila mwisho wa msimu.

“Ni kweli Simba wameonesha nia ya kutaka huduma zangu, lakini katika kipindi hiki sipendi kuzungumza chochote kuhusu uamuzi wangu kuhusu suala hilo,” alisema Hassan, ambaye alishinda tuzo ya Mchezaji Bora wa mwaka wa klabu wa Januari. Alisema kuwa ana furaha kwa wote waliomuunga mkono hadi kuwa mchezaji bora, na hasa kupata nafasi ya kuichezea timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars.

“Napenda kushukuru wachezaji wenzangu kwa ushirikiano ambao wamekuwa wakiutoa kwangu, benchi la ufundi kwa mazoezi mazuri na siwezi kuwasahau viongozi wa klabu kwa kile walichofanya kututia moyo ili tuweze kucheza soka vizuribila matatizo yoyote,” alisema.

Mashabiki wa Pwani wa klabu hiyo wamewataka viongozi wa Bandari kuhakikisha wachezaji wote wanabaki kwa ajili ya msimu wa mwaka 2019-2020. Hassan pia alikanusha taarifa kuwa amekuwa akitakiwa na mabingwa wa Kenya Gor Mahia. “Sina hizo taarifa kwa sababu sijawahi kuzungumza na kiongozi yeyote wa Gor na wengine, siwezi kusema kama kuna ukweli wowote katia taarifa hizo, “alisema.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/e45b9bdb9140836b944d419c6f5656fd.jpg

MAKOCHA wa Simba Pablo Franco na wa Yanga, ...

foto
Mwandishi: MOMBASA, Kenya

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi