loader
Picha

Queen Darleen: Diamond na Ali Kiba freshi mbona

MSANII wa muziki wa kizazi kipya Mwajuma Abdul maarufu Queen Darleen amedai kuwa ukaribu wake na Msanii Ali Kiba umepungua kutokana na majukumu ya kifamilia aliyonayo.

Aidha amekanusha taarifa kuwa Msanii Diamond Platinumz ambaye ni mdogo wake na Ali Kiba hawaiivi na kwamba kama ingekuwa hivyo nyimbo za Ali Kiba zisingepigwa Wasafi Media.

Akizungumza kwenye moja ya mahojiano aliyoyafanya hivi karibuni, Queen Darleen alisema kuwa majukumu ya kifamilia yanasababisha wakati mwingine mtu apunguze ukaribu na mwingine kwani kila mmoja anakuwa na harakati zake za kusaka maisha.

“Unajua maisha yamebadilika tulikuwa watoto, lakini mwisho wa siku kila mtu kagawanyika na majukumu yake Ali ameowa na yupo na familia yake kwa hiyo kila mtu na maisha yake,” alisema Queen Darleen na kusisitiza kuwa ni majukumu tu yanayowaweka mbali.

Queen Darleen na Ali Kiba waliwahi kufanya kazi pamoja miaka 12 iliyopita walipotoa nyimbo inayoitwa 'Wajua' ambayo ilifanya vizuri.

 

SIMBA na Yanga ni miongoni mwa klabu kongwe zinazotajwa kupata ...

foto
Mwandishi: Rahimu Fadhili

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi