loader
Picha

Mapro Ligi Kuu Bara na timu zao Afcon

MASHINDANO ya Ligi Daraja la Kwanza imemalizika hivi karibuni na timu zilizofanikiwa kupanda na kucheza Ligi Kuu zimejulikana na timu zilizoshuka daraja nazo zinajulikana pia.

Lengo la makala haya si kueleza timu zilizopanda na kucheza Ligi Kuu na sio kueleza timu zilizoshuka daraja bali dhumuni kubwa ni kutaka kuweka wazi zababu zilizosababisha Arusha United maarufu kwa jina la ‘’Wana Utalii’’ kupanda kisoka na hatimaye kupwaya katika ligi hiyo wakati ni moja ya timu iliyokuwa ikipewa nafasi kubwa ya kufanya vizuri.

Arusha United ilizaliwa baada ya uongozi wa mkoa chini ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo kuamua kuchukuwa jina la JKT Oljoro iliyokuwa Daraja la Kwanza na kuibadilisha jina na kuwa Arusha United, lengo ni kutaka timu hiyo kupanda daraja na hatimaye kucheza Ligi Kuu, kwani malengo ya kiongozi huyo wa mkoa yalikuwa mazuri kwa maslahi ya wakazi wa Arusha, lakini malengo hayo hayakutimia.

Mkuu huyo alikuwa na mawazo mazuri kwanza timu hiyo kwani ikipanda daraja uchumi kwa wafanyabiashara wa Mkoa wa Arusha utakuwa na pili ni kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika michezo malengo ambayo yalikubalika ipasavyo na kuungwa mkono na wakazi wa Jiji la Arusha na vitongoji vyake.

Arusha United sio timu ya kwanza mkoani Arusha ya kiraia mbali ya AFC, lakini ni timu iliyokuwa na uongozi madhubuti na timu ilikuwa na uwezo wa kifedha kwa sababu ilikusanya pesa nyingi za uendeshaji na usajili kutoka kwa wafanyabiashara mkoani Arusha na ilikuwa ikijiendesha kisasa zaidi tofauti na timu zilizowahi kutamba huko nyuma kama AICC, Ndovu, Kiltex na Jumuiya.

Ukiachilia mbali jitihada za Gambo aliyekuwa mstari wa mbele kuhakikisha timu hiyo inafanikiwa kupanda daraja na kuamuwa kujitoa kwa dhati kufanikisha lengo hilo, timu hiyo ilikamilikia kila idara ikiwa ni pamoja na kuwa na Mtendaji Mkuu (CEO), Bodi ya Wakurugenzi, benchi la ufundi na Msemaji wa timu.

MATUMAINI KIBAO

Arusha United ilianza ligi kwa kishindo na kufanya vema katika michezo mingi ya raundi ya kwanza na kushika nafasi ya pili na ya kwanza hadi raundi hiyo inamalizika na kuonesha matumaini kwa wakazi wa Mkoa wa Arusha kuwa msimu ujao huenda wakaona Ligi Kuu. Hali ilikuwa tofauti kwa hatua ya raundi ya pili, kwani timu hiyo ilianza kufanya vibaya na viongozi kuanza kutimuana kwa kuanzia

MKUU wa Mkoa wa Songwe, Nicodemus Mwangela ametoa siku saba ...

foto
Mwandishi: John Mhala, Arusha

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi