loader
Picha

Majaliwa mgeni rasmi Kubwa Kuliko leo

WAZIRI Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa leo anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye kilele cha harambee ya kuichangia klabu ya Yanga itakayofanyika kwenye ukumbi wa Daimond Jubilee Dare es salaam.

Mbali na mgeni rasmi huyo harambee hiyo pia inatarajiwa kuhudhuriwa na Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Mrisho Kikwete huku likinogeshwa na wasanii mbalimbali wa kizazi kipya ambao ni mashabiki wa timu hiyo.

Harambee hiyo ya awamu ya pili iliyopewa jina la Kubwa Kuliko imeandaliwa kuratibiwa na kamati ya kuhamasisha wanachama na wapenzi wa timu hiyo inayoongozwa na mwenyekiti wake, ambaye ni Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Anthony Mavunde.

Kwenye uzinduzi wa kampeni awamu ya kwanza iliyofanyika mkoani Dodoma iliyongozwa na kocha wa timu hiyo Mwinyi Zahera kamati hiyo ilifanikiwa kukusanya kiasi cha sh. Milion 500 kati ya kiasi cha Bilion 1.5 wanachotarajia kukipata.

’Kubwa kuliko’ tukio linalotajwa litavunja rekodi kulishinda lile la awamu ya awali ambapo fedha takayopatikana itaisaidia timu hiyo kufanya usajili wa wachezaji wa maana kwa ajili ya kusuka kikosi kipya kwa ajili ya kuleta ushindani katika mechi za ligi ya ndani na kimataifa.

Kwa mjibu wa mwenyekiti wa Kamati Ndogo ya kuhamsisha wanachama na wapenzi kuichangia timu hiyo David Luhaga alisema maandalizi ya kuelekea kwenye tukio hilo kubwa yamekamilika hivyo amewaomba wanayanga kujitokeza kwa wingi kuunga mkono zoezi hilo.

“Tunawaomba wanachama na wapenzi wajitokeze tumefanya maandalizi makubwa ikiwemo kuwaalika viongozi wakubwa kuchagiza tukio hili na kwa wale walioko mikoa mbalimbali waende kwenye matawi wakachangie tumeweka utaratibu makini wa kuhakikisha kila kinachotolewa kinatufikia,” alisema Luhaga.

KOCHA wa timu ya Soka ya wanawake ya Tanzania ‘Twigar ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi