loader
Wabunge kuisapoti Stars Misri

Wabunge kuisapoti Stars Misri

SPIKA wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai pamoja na wabunge 83, watanogesha na kuipa joto timu ya Tanzania ,Taifa Stars, kwenye fainali za 32 za Mataifa ya Afrika, Afcon 2019, zitakazonza Misri Juni 21 hadi Julai 17.

Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini hapa, Mwenyekiti wa Klabu ya Michezo ya Bunge, William Ngeleja alisema katika kuipa joto timu ya Taifa Stars, wabunge 83, wakiongozwa na Spika Ndugai watakwenda Misri kuishangilia timu hiyo.

Ngeleja alisema Bunge limetafakari na kuona umuhimu wa kuipa hamasa timu ya Tanzania, hasa baada ya kupata nafasi hiyo baada ya miaka 39, hivyo wabunge hao wataenda kuishangilia ili kuipa nguvu ya kushinda.

“Tunaishukuru Serikali na Bunge pamoja na kazi kubwa iliyombele yetu hivi sasa ya mkutano wa Bunge la Bajeti, lakini imeonekana pia ni vyema kukaenda kuishangilia timu yetu kule Misri, na tutaenda kwa awamu mbili ili kutoa nafasi pia kwa wabunge kuchangia mjadala wa bajeti ya Serikali,” alisema Ngeleja.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/baa414becaed6d1066dcbfd36ddeaad0.jpg

WAFANYABISHARA mbalimbali wa Temeke, ...

foto
Mwandishi: Ikunda Erick, Dodoma

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi