loader
Picha

Nigeria yamtema nyota EPL

NIGERIA imetangaza majina ya wachezaji 23 kwa ajili ya fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon 2019) nchini Misri, akiwemo mchezaji wa Kaizer Chiefs, lakini imemtema nyota wa Ligi Kuu ya England.

Mshambuliaji wa Leicester City Kelechi Iheanacho (pichani) alitangazwa katika kikosi cha awali cha kocha Gernot Rohr cha wachezaji 25 kwa ajili ya maandalizi ya mashindano hayo, lakini alitemwa katika kikosi cha mwisho, pamoja na wachezaji wengine wawili.

Mwingine aliyeondolewa katika kikosi hicho ambacho kitashiriki mashindano hayo Misri ni kiungo Semi Ajayi, ambaye anayechezea timu ya Daraja la Kwanza ya England ya Rotherham United.

Wengi wa wachezaji hao 23 walikuwemo katika kikosi cha Rohr ambacho kilishiriki Kombe la Dunia nchini Russia mwaka jana. Wachezaji hao ni pamoja na Ahmed Musa, Wilfred Ndidi, Alex Iwobi, Leon Balogun na kiungo mkongwe John Mikel Obi, ambaye atakuwa na nahodha wa Nigeria baada ya kurejea katika timu hiyo baada ya kikao na kocha.

Winga wa Villarreal Samuel Chukwueze na mshindi wa Kombe la Dunia kwa wachezaji wenye umri wa chini ya miaka 17 mwaka 2015 Victor Osimhen nao pia wote wameitwa katika kikosi hicho, ambao wanashiriki kwa mara ya kwanza katika timu ya wakubwa. Kikosi cha Rohr kilitoka suluhu na Zimbabwe katika mchezo wa kirafiki uliofanyika Asaba Jumamosi, na sasa itatua Misri tayari kwa mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Senegal Juni 16.

Mabingwa hao mara tatu wa Afcon wamepangwa katika Kundi B, pamoja na Guinea, Madagascar na Burundi. Super Eagles itacheza dhidi ya Burundi Juni 22 katika mchezo utakaofanyika kwenye Uwanja wa Alexandria mjini Alexandria.

Kikosi kamili: Makipa: Francis Uzoho (Anorthosis Famagusta, Cyprus); Ikechukwu Ezenwa (Katsina United); na Daniel Akpeyi (Kaizer Chiefs, Afrika Kusini) Mabeki: Olaoluwa Aina (Torino, Italia); Abdullahi Shehu (Bursaspor, Uturuki); Chidozie Awaziem (Rizespor, Uturuki); William Ekong (Udinese, Italia); Leon Balogun (Brighton, England); Kenneth Omeruo (CD Leganes, Hispania); Jamilu Collins (SC Padeborn 07, Ujerumani) Viungo: John Mikel Obi (Middlesbrough, England); Wilfred Ndidi (Leicester City, England); Oghenekaro Etebo (Stoke City, England); John Ogu (Hapoel Be’er Sheva, Israel) Washambuliaji: Ahmed Musa (Al Nassr, Saudi Arabia); Victor Osimhen (Royal Charleroi, Ubelgiji); Moses Simon (Levante, Hispania); Henry Onyekuru (Galatasaray SK, Uturuki); Odion Ighalo (Shanghai Shenhua, China); Alexander Iwobi (Arsenal, England); Samuel Kalu (Girondins Bordeaux, Ufaransa); Paul Onuachu (FC Midtjylland, Denmark); Samuel Chukwueze (Villarreal, Hispania).

MKUU wa Mkoa wa Songwe, Nicodemus Mwangela ametoa siku saba ...

foto
Mwandishi: LAGOS, Nigeria

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi