loader
Picha

Wanawake wagoma wakitaka usawa mishahara

WANAWAKE nchini hapa wamefanya mgomo kazini kupinga kile wanachodai ni kutokuwapo usawa wa kijinsia hususani katika mishahara. Hawakwenda kazini badala yake waliandamana mtaani pamoja na kwenda mbele ya jengo la serikali mjini Bern kushinikiza mabadiliko.

Mgomo huo wa jana umekuja miaka 28 baada ya kufanyika mwingine wa namna hiyo mwaka 1991 uliohusisha wanawake wapatao 500,000 . Wanawake nchini wamekuwa katika kampeni ya muda mrefu kuharakisha usawa wa kijinsia. Waliungana na mamilioni ya wanawake wa Ulaya baada ya Vita ya Kwanza ya Dunia iliyomalizika mwaka 1918 wakitaka haki ya kupiga kura ambayo hawakuipata hadi 1971.

Wakati wa mgomo mwaka 1991, hapakuwapo mwanamke yeyote aliyekuwa katika serikali ya Uswisi na pia hapakuwa na sheria yoyote ya kuruhusu wanawake kwenda likizo ya uzazi. Mpaka sasa, wanawake nchini Uswisi hupata asilimia 20 pungufu ya kipato cha wanaume. Pia wana uwakilishi mdogo nafasi za juu uongozi. Mwezi uliopita, utafiti wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) uliiweka Uswisi nafasi ya chini ya orodha ya nchi zinazolipa kiwango kidogo kati ya wanawake na wanaume majukumu ya juu.

“Nafikiri baada ya hapa, hakuna kitu kitakachoshindikana,” alisema mwandishi wa habari, Beatrice Born ambaye mwaka 1991 alipokwenda kujifungua, aliporudi kazini hakutakiwa kuendelea na kazi yake. Mmoja wa waratibu wa mgomo wa mwaka 1991, Paola Ferro, alisema anashiriki mgomo huu mpya na sababu za kufanya hivyo ni haki ya kijinsia kama ilivyokuwa miaka 28 iliyopita.

Ingawa alisema yapo mabadiliko yaliyotokana na mgomo huo wa awali, lakini alisema suala la malipo na utofauti katika pensheni ni masuala mengine ambayo wanataka yapatiwe ufumbuzi. Pensheni kwa wanawake wa Uswisi iko chini kwa asilimia 37 kuliko wanaume kwa sababu wanawake huchukua muda mrefu wakiwa nje ya kazi kwa sababu ya kulea watoto wachanga.

Miongoni mwa wanawake waliohojiwa na vyombo vya habari walisema hii ni fursa nzuri ya kusimama pamoja kuonesha hawafurahii mambo yanavyokwenda ikiwamo wasichana kupewa nafasi chache kuendelea na elimu ya juu. Imeelezwa maelfu ya wanawake wameshaarifu wakuu wao wa kazi hawatakwenda kazini na wengine wataondoka mapema kuandamana. Baadhi ya waajiri walisema mgomo huo ni batili. Lakini baadhi ya wanaume wanaunga mkono mgomo huo wakisema haki itendeke.

MKUU wa Mkoa wa Songwe, Nicodemus Mwangela ametoa siku saba ...

foto
Mwandishi: BERN, Uswisi

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi