loader
Picha

Baba: Haji Manara kazaliwa na kulelewa Yanga, asiwasumbue

MCHEZAJI wa zamani wa Klabu ya Yanga, Sunday Manara amesema mtoto wake ambaye ni Msemaji wa Klabu ya Simba, Haji Manara amelelewa na kukulia Yanga.

Kwa mantiki hiyo, Sunday Manara ‘Computer’ amewataka wananchama na mashabiki wa Yanga wasisumbuliwe na mwanaye huyo ambaye amekuwa akitoa utani dhidi ya klabu hiyo ya Jangwani.

Mchezaji huyo wa zamani wa Yanga na Taifa Stars ametoa kauli hizo leo katika hafla ya kuichangia Klabu ya Yanga iliyopewa jina ‘Kubwa Kuliko’ yenye dhamira ya kukusanya Sh. bilioni 1.5.

Baba yake Haji Manara ameshauri kuwa wachezaji wa zamani waliolitumikia taifa kwa muda mrefu wapewe heshima ya kushauri na hata kuruhusiwa kuingia kwenye viwanja vya michezo bure.

Mgeni rasmi wa tukio hilo ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa huku Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akiwa ni mgeni maalum katika shughuli hiyo.

Viongozi wengine wa kitaifa wakiwemo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda wamehudhuria tamasha hilo linaloendelea katika Ukumbi wa Diamond Jubilee.

KOCHA wa timu ya Soka ya wanawake ya Tanzania ‘Twigar ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi