loader
Picha

Mikoa 8 yapewa mwaka mmoja kukamilisha mwongozo uwekezaji

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa ametoa mwaka mmoja kwa viongozi wa mikoa minane kukamilisha kuandaa mwongozo wa uwekezaji katika maeneo yao.

Pia ameliagiza Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) kuratibu mifuko yote ya uwezeshaji wananchi kiuchumi ikiwa ni ile ya binafsi na serikali na taarifa zake kupelekwa kwake. Majaliwa alitoa maagizo hayo jana jijini hapa wakati akifungua Kongamano la Nne la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi.

Kongamano hilo limeandaliwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) huku kaulimbiu yake ni Wezesha Watanzania Kujenga Viwanda na Kampuni ya Tanzania Standard Newspapers (TSN) Limited ikiwa ni moja ya wadhamini wa kongamano hilo. Alisema mikoa hiyo minane ambayo haijakamilisha mwongozo wa uwekezaji kufanya hivyo na ile ambayo tayari imeshakamilisha mwongozo kuhakikisha inatoa taarifa za utekelezaji wake mwakani wakati wa kongamano la tano. Mikoa hiyo minane ni Dar es Salaam, Morogoro, Iringa, Njombe, Mbeya, Rukwa, Singida na Shinyanga.

“Mikoa ambayo haijaandaa mwongozo wa uwekezaji kuhakikisha inafanya hivyo ili fikapo mwakani kuwe na taarifa na pia mikoa yote iliyokamilisha kuandaa mwongozo wa uwekezaji, nayo ifikapo mwakani inapaswa kuonesha hatua za utekelezaji katika kuainisha mikakati ya kuzitangaza fursa katika maeneo yao na kuzitumia,” alisema. Pia ameliagiza Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kuratibu mifuko yote ya uwezeshaji wananchi kiuchumi ikiwa ni ile ya binafsi na serikali na apelekewe taarifa.

“Baraza la Taifa la Uweze- shaji Wananchi Kiuchumi hakikisheni mratibu kwa karibu mifuko yote ya uwezeshaji wananchi kiuchumi ikiwa ni ile ya binafsi na ile ya serikali ili kujua iko mingapi, inawanufaisha akina nane na je wanafuaika wanajijua… kwa mifuko ya serikali nataka kujua ijulikane iko mingapi, inawanufaisha akina nani na je, wanafufaika wanajijua? “Ili serikali ije na maamuzi kama ya kuunganisha mifuko ili kuwa michache na itoe huduma yenye tija na taarifa niletewe.

Lakini kwa ile ya binafsi, pia tujue ipo mingapi na inamnufaisha nani na je wanufaika wanajijua na ni kweli wananufaika, lango ni kuhakikisha huduma inayotolewa iwe na uhalisia,” alisema Waziri Mkuu. Aidha, Majaliwa pia aliwaagiza viongozi wa mikoa na halmashauri zote nchini kuhakikisha wanaanzisha vituo vya uwezeshaji wananchi kiuchumi kama kile cha Kahama ili kuharakisha nia ya serikali katika kuwezesha wananchi kiuchumi.

“Leo hii kituo hiki (cha Kahama) kimekuwa na tija kubwa kwa sababu nchi za jirani za Burundi na Rwanda walikuwa wanafanya manunuzi yao Tanzania na kulazimika kwenda hadi Dar es Salaam katika soko la Kariakoo kupata huduma. Lakini safari imerahisishwa kwa sababu wamekuwa wakifanya manunuzi katika kituo hiki na kwa safari ya siku moja,” alisema.

Waziri Mkuu Majaliwa pia aliagiza Baraza kutumia matokeo ya tafiti ziliyofanywa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) ili kuja na maandiko ya miradi mikubwa ambayo itasaidia kuinua wananchi kiuchumi. “Niziagize mamlaka zote kushirikiana na NEEC kuhakikisha kuwa fursa za uwezeshaji wananchi kiuchumi zilizobainishwa kupitia tafiti za UNDP zinafanyiwa kazi. Pia hakikisheni kuwa miradi mikubwa ya uwezeshaji wananchi kiuchumi inatokana na tafiti hizo,” alisema.

Majaliwa alisema serikali inatambua tafiti zilizofanywa na UNDP kuhusu biashara na uwekezaji nchini yanatarajiwa kuchangia kwa kiasi kikubwa katika uandaaji wa maandiko ya miradi mikubwa inayopendekezwa na shirika hilo. “Miradi hiyo ni pamoja na ule wa “Harmonized Innovation Solutions for Local Economic Development” ambao upo katika hatua za maandalizi.

Lengo la UNDP ni kuhakikisha kuwa miradi inayohusu uwezeshaji wananchi kiuchumi inatekelezwa moja kwa moja na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ambalo lipo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu.” Alisema Baraza lina uwezo mkubwa katika kusimamia miradi mbalimbali ya uwezeshaji ambayo imekuwa ikifadhiliwa na Serikali pamoja na Jumuiya ya Kimataifa ikiwemo UNDP, ILO, UNCTAD, AfDB na UN- Women, hivyo ameyahakiki- shia mashirika hayo kuwa Serikali itasimamia kikamilifu utekelezaji wa miradi yote ili kupata matokeo yaliyo tarajiwa.

Majaliwa alionesha imani kubwa kuwa kupitia utekelezaji wa miradi hiyo, malengo mbalimbali ya nchi kuhusu uwezeshaji wananchi kiuchumi yatafikiwa. Baadhi ya malengo hayo ni pamoja na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2015 - 2020; Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano; Dira ya Taifa ya Miaka 25; na Malengo Endelevu ya Maendeleo ya umoja wa Mataifa (SDGs).

Waziri Mkuu pia ameli- taka Baraza la Taifa la Uweze- shaji Wananchi Kiuchumi liendelee kuratibu masuala ya uwezeshaji wananchi kiuchumi ikiwemo utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa kipindi cha 2015 - 2020 kuhusu uanzishwaji wa viwanda vidogo, vya kati na vikubwa vya kuchakata mazao ya kilimo, mifugo, uvuvi na misitu. “Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi iboresh- we sambamba na kuongeza ufanisi ili iweze kuwafikia Watanzania wengi hususan wale wa vijijini.

Vilevile, kamilisheni na hakikisheni mnazindua haraka mfumo wa kupima mifuko ya uwezeshaji kwa matokeo ya kiuchumi na kijamii na siyo kwa shughuli walizofanya,”alisema.

Alisema uwezeshaji wananchi kiuchumi ni suala mtambuka, sekta mbalimbali za kiuchumi na sekta binafsi zinajihusisha moja kwa moja katika kuwawezesha wananchi kiuchumi na kusisitiza umuhimu wa masuala ya uratibu, ufuatiliaji na tathimini ya shughuli za uwezeshaji wananchi kiuchumi, yakafanywa mara kwa mara ili kuweza kufikia malengo waliyojiwekea.

MKUU wa Mkoa wa Songwe, Nicodemus Mwangela ametoa siku saba ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike, Dodoma

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi