loader
Picha

Serikali yapokea vifaa kinga ebola seti 3,500

SERIKALI imepokea jumla ya seti 3,500 za vifaa kinga kwa ajili ya watumishi wa afya kupitia ofi si za Kanda za Bohari Kuu ya Dawa nchini (MSD) kwa ajili ya kujiandaa na tishio la sasa la mlipuko wa ugonjwa wa ebola.

Hayo yalibainishwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wa- zee na Watoto, Ummy Mwalimu jana katika Manispaa ya Ilemela mkoani hapa wakati alipokuwa akitoa taarifa ya tahadhari kwa umma kuhusu tishio la mlipuko wa ugonjwa huo kwa wananchi ambao umeripotiwa kuwepo katika nchi ya Kidemokrasia ya Kongo(DRC) na kwa sasa nchini Uganda.

Alisema kutokana na tishio la sasa la ugonjwa huo, serikali itaongeza jumla ya seti nyingine 4,000 itakapozipeleka karibu zaidi na wananchi, ikiwa ni pamoja na kwenye hospitali zote za mikoa na wilaya kwa ajili ya kuziwezesha kwa ajili ya tishio la ugonjwa huo.

Waziri Ummy alisema mbali na seti hizo, serikali pia imeandaa kitini chenye maelezo muhimu ya kukabiliana na ugonjwa huo ambapo nakala tete zimetumwa kwa waganga wakuu wa mikoa na kwamba serikali itaendelea kudurufu nakala zaidi zitaka- zosambazwa kwa kila mkoa, wilaya, vituo vya afya hapa nchini kwa ajili ya kutumiwa na watumishi wa afya na wananchi ambapo vitatumika kwa ajili ya kutoa elimu kwa umma.

“Tumefanya tathimini ya kupima utayari wa mikoa na halmashauri katika maeneo yaliyoainishwa kuwa na hatari zaidi ya kupata wagonjwa wa ebola kutoka nchi jirani. Maeneo ya kufanyiwa kazi yameainishwa na jitihada za kuyaondoa mapungufu zinaendelea,” alisema.

Aliongeza kuwa serikali imetoa mafunzo kwa watumishi zaidi ya 460 wa sekta ya afya na 264 kutoka ngazi ya jamii (viongozi wa dini, wanahabari, bodaboda pamoja na watendaji wa vijiji) katika mikoa iliyo na hatari kubwa zaidi ya maambukizi ya ugonjwa huo ambapo mpango huo wa mafunzo utakuwa ni endelevu.

Alisema pia serikali imeimarisha utambuzi wa ugonjwa huo kwa kujenga uwezo hapa nchini katika Maabara Kuu ya Taifa iliyoko jijini Dar es Salaam, hospitali ya rufaa kanda ya Mbeya na Taasisi ya Utafiti ya Kiliman- jaro iliyopo Moshi sanjari na kuboresha mfumo wa usafirish- aji wa sampuli kwenda katika maabara hizo kwa uthibitisho na uchunguzi.

“Nimeagiza iletwe maabara moja ya kutembea hapa Bugando kwa ajili ya jambo hili na niwaambie wananchi kuwa kuwepo kwa ugonjwa wa ebola sio tatizo, tatizo ni ugonjwa kusambaa na sisi tumejipanga vizuri kuudhibiti endapo utatokea,” alisema. Aliiagiza mikoa na halmashauri zote nchini kuimarisha mfumo wa ufuatiliaji wa magonjwa ya milipuko na kutoa taarifa za wiki kwa wakati na za siku pale inapobidi kwa ajili ya udhibiti.

Ukubwa wa tatizo Waziri Ummy ambaye pia alipata fursa ya kukagua majengo maalumu yaliyojengwa katika manispaa ya Ilemela kwa ajili ya maandalizi ya kupokea wagonjwa endapo watabainika kuwepo nchini, alisema jumla ya watu 2,108 wamethibitika kuwa na ugonjwa wa ebola katika nchi ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ambapo kati ya hao, watu 1,411 wameripotiwa kufariki na watu 585 ambao ni washukiwa wa ugonjwa huo wanaendelea kufanyiwa uchunguzi.

Alisema ugonjwa huo pia umeripotiwa kutokea katika nchi jirani ya Uganda katika wilaya ya Kasese iliyopo upande wa Kusini Magharibi mwa nchi hiyo, ambapo kwa upande wa Tanzania wilaya hiyo inapakana na wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera na kuwa Juni 11, mwaka huu, mtoto mwenye umri wa miaka mitano alithibitika kuwa na ugonjwa wa ebola baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kimaabara, ambaye alifariki dunia siku iliyofuata.

Aidha, watu wengine wawili kutoka kwenye familia ya mtoto huyo wamethibitishwa kuwa na ugonjwa huo Juni 12 mwaka huu na hivyo kufanya idadi ya watu watatu walioa na maambukizi ya ugonjwa huo na kuwa hali hiyo ilisababisha Wizara ya Afya nchini Uganda na Shirika la Afya Duniani (WHO) kutangaza rasmi uwepo wa mlipuko wa ugonjwa huo nchini humo Juni 11 mwaka huu. “Kufuatia taarifa hiyo, kunafanya nchi za Uganda na DRC kuwa na mlipuko wa ugonjwa huu,” alisema na kuongeza kuwa kuwepo kwa ugonjwa huo nchini Uganda kunaongeza hatari zaidi ya ugonjwa huo kuingia hapa nchini.

MKUU wa Mkoa wa Songwe, Nicodemus Mwangela ametoa siku saba ...

foto
Mwandishi: Nashon Kennedy, Mwanza

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi