loader
Picha

Vikundi 53 vya vijana Lindi vyapewa mil 200/-

OFISI ya Waziri Mkuu inayoshughulikia Sera, Bunge, Vijana, Kazi na Ajira mkoani Lindi imetoa mikopo yenye thamani ya Sh milioni 200 kwa vikundi vya uzalishaji mali vya vijana tujiajiri 53 kwa nyakati tofauti.

Vijana hao wanatoka vikundi vya uzalishaji vilivyoko katika halmashauri sita za wilaya za Kilwa, Liwale, Nachingwea, Lindi, Ruangwa na Manispaa ya Lindi mkoani humo. Ofisa Maendeleo ya Vijana, Ofisi ya Waziri Mkuu inayoshughulikia Sera, Bunge, Vijana, Kazi na Ajira kutoka makao makuu mkoani Dar es Salaam, Atupokile Mhalila alisema hayo jana wakati alipokuwa akizungumza kwa nyakati tofauti na vikundi mbalimbali vya uzalishaji.

Mhalila alisema mikopo hiyo imegawanyika katika sehemu kuu mbili, kwanza kuanzisha miradi na pili kuendeleza vijana wanaounda makundi hayo. Mhalila alisema lengo kuu ni kuwanyanyua vijana kiuchumi kwa kuanzisha miradi ya uzalishaji mali ili iwawezeshe kujiajiri wenyewe na kupata kipato kwa kuanzisha viwanda vidogo. Alisema kila kikundi kinakuwa na vijana kumi na hupewa mkopo baada ya kuomba mradi wanaotaka kuufanya na kuutekeleza.

Ofisa Maendeleo ya Jamii katika Manispaa ya Lindi, Iddi Maketa alisema kuwa wizara ya nchi, ofisi ya waziri mkuu inayoshughulikia sera, kazi, bunge, ajira na vijana ilitoa mikopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Lindi kiasi cha Sh milioni 90 kwa vipindi tofauti, navyo ni 2014/15, 2016/17 na 2018. Alisema vikundi vya hapa mjini vinajishughulisha kuongezea thamani mbao kwa kutengeneza samani za viti, vitanda na aluminium kwa madirisha, ya vioo na uchomoleaji wa milango ya vyuma pamoja na madirisha yake.

Abdul Said kutoka kikundi cha Mshikamano cha kata ya Wailes mjini hapa aliishukuru serikali kwa kuwapa mkopo wa Sh 3,000,000 na uliwawezesha wanachama watano. Alisema walitumia fedha hizo kununua mashine za kuchomea na vifaa vinginevyo vya mradi wao wa kikundi hicho na kutoa ushauri kwa serikali badala ya kutoa fedha za mkopo wakopeshe vifaa vya kufanyia kazi siyo kutoa mkopo wa fedha.

MKUU wa Mkoa wa Songwe, Nicodemus Mwangela ametoa siku saba ...

foto
Mwandishi: Kennedy Kisula, Lindi

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi