loader
Picha

Baba ahukumiwa kunyongwa kwa kuua watoto watano

MWANAMUME aliyekuwa akikabiliwa na mashitaka ya kuua watoto wake watano nchini hapa, Tim Jones amehukumiwa kunyongwa. Mahakama imemhukumu kunyongwa mpaka kufa huku ikitupilia mbali ombi la mkewe, mama wa watoto hao la kutaka asamehewe.

Mama huyo, Amber Kyzer alidai anaomba mumewe asinyongwe kwa niaba ya watoto wake. Awali, Kyzer aliiambia mahakama baba huyo mwenye umri wa miaka 37 hakuonesha huruma kwa watoto ingawa alidai watoto walimpenda. “Watoto walimpenda; endapo nitaongea kwa niaba yao, basi kitu pekee nitakachosema kutoka kwao ni kumwombea msamaha,” alidai.

Jones alikiri alimfanyisha mazoezi magumu mtoto wake mkubwa akadondoka na kufa. Baada ya hapo aliwanyonga wanne waliosalia mmoja baada ya mmoja, na kupakia miili yao kwenye gari. Aliendesha gari kwa siku tisa. Alisema aliitupa miili ya watoto hao kwenye matangi ya taka kwenye jimbo la Alabama. Inaelezwa kuwa watoto hao walikuwa na umri wa kati ya miaka minane na mwaka mmoja.

Hukumu ya kunyongwa hadi kufa ilitolewa baada ya waendesha mashitaka kudai hukumu ya kifungo cha maisha jela itakuwa ni sawa na kumpeleka Timmy chumbani kwake. Inaelezwa kwamba Jimbo la South Carolina halijanyonga mfungwa tangu mwaka 2011. Baba huyo alitiwa hatiani kwa mauaji ya watoto wa mwaka mpaka miaka minane mwaka 2014.

Pamoja na mama wa watoto, Amber kuomba mahakama isimhukumu kifo, wazee wa baraza walitakiwa kufikia uamuzi wa pamoja. Wazee hao wa baraza, saba wakiwa wanaume na wanawake watano, baada ya saa mbili za majadiliano, walikubaliana ahukumiwe kunyongwa. Wangetofau- tiana Jones angehukumiwa kifungo cha maisha jela. Waendesha mashi- taka waliwataka wazee wa baraza kukumbuka ni kwa namna gani mwanaume huyo aliwaua watoto wake hao.

MKUU wa Mkoa wa Songwe, Nicodemus Mwangela ametoa siku saba ...

foto
Mwandishi: SOUTH CAROLINA, Marekani

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi