loader
Picha

Papa Francis aonya ongezeko la joto

KIONGOZI wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis amewaambia viongozi wa mashirika ya kimataifa yanayozalisha na kusambaza bidhaa za mafuta na gesi zinazotoa hewa ukaa kuwa biashara ya hewa ukaa ni muhimu kudhibitiwa kwa kutozwa kodi ili kuzuia ongezeko la joto.

Amewataka wasiokubaliana na mabadiliko ya tabia nchi wasikilize sayansi inavyosema sasa. Papa Francis alisema hayo juzi Vatican kuunga mkono kuadhibu watu wanaochafua mazingira na kusababisha mabadiliko ya tabia nchi. Wakati akihutubia watendaji wa masuala ya nishati baada ya mkutano wa siku mbili, Papa alitaka yatolewe maelezo ya wazi, kisayansi na yaliyo katika viwango vinavyokubalika kuhusu hatari katika tabia nchi ili kuokoa dunia.

Kuongezeka kwa joto duniani ni matokeo ya ongezeko la hewa ukaa angani linalochangiwa na shughuli mbalimbali za kibinadamu. Biashara ya hewa ya ukaa kupitia kodi kwa makampuni yanayozalisha, kusambaza bidhaa zinazotoa hewa ukaa hutumiwa na serikali nyingi kutoza watumiaji wa nishati gharama za kutumia mafuta yanayochangia joto duniani.

Mkutano huo wa ndani ulihusisha wakurugenzi watendaji kutoka Royal Dutch Shell, Eni, BP, Repsol, Conoco Phillips, Chevron, ExxonMobil na watendaji wa mifuko ya uwekezaji. Rais wa Chuo Kikuu cha Notre Dame, Marekani aliyeandaa mkutano huo, John Jenkins alisema viongozi hao wana uwezo wa kufanya maboresho kwa hatma ya sayari ya dunia.

Wakati mkutano ukien- delea, nje ya lango la Vati- can kulikuwa na kikundi cha waandamanaji wakiwa na bango lililoandikwa ‘wapendwa watendaji wakuu wa mafuta, fikiria watoto wetu.’ Papa Francis amekuwa akitoa mwito mara kwa mara kuhusu suala zima la ulinzi wa mazingira.

MKUU wa Mkoa wa Songwe, Nicodemus Mwangela ametoa siku saba ...

foto
Mwandishi: VATICAN, Italia

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi