loader
Picha

Stars kibaruani na Zimbabwe leo

TIMU ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, leo inashuka uwanjani nchini Misri kucheza mechi ya kirafi ki na timu ya taifa ya Zimbabwe kujipima ubavu kabla ya kuanza michuano ya Mataifa ya Afrika (Afcon 2019).

Mchezo huo ni wa pili kwa Stars iliyopo katika Kundi C pamoja na timu za Senegal, Algeria na Kenya baada ya Alhamisi iliyopita kucheza na wenyeji wa michuano hiyo Misri na kukubali kipigo cha bao 1-0.

Zimbabwe iliyo Kundi A pamoja na timu za Misri, DR Congo pamoja na Uganda, itatupa karata yake ya kwanza katika mchezo wa ufunguzi Juni 21 dhidi ya Misri. Kocha wa Stars, Emmanuel Amunike amepan- ga kukipima kikosi chake kwa mechi mbili kabla ya kuanza kwa mikikimikiki ya Afcon ili kujua uimara na udhaifu wa kikosi chake.

Akizungumza hivi karibuni alisema kuwa amechagua kucheza mechi za kirafiki dhidi ya timu hizo ngumu, kwani zinamfanya kujua mapungufu yaliyopo katika kikosi chake. “Tunaweza kujirekebi- sha makosa yetu yaliyopo kabla ya kuanza katika mechi yetu ya kwanza ya Afcon, kucheza na timu ngumu ni chachu kwetu kuweza kupambana na kuonesha kitu tulichonacho,” alisema Amunike.

KOCHA wa timu ya Soka ya wanawake ya Tanzania ‘Twigar ...

foto
Mwandishi: Mohammed Mdose

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi