loader
Picha

‘Kila timu inafikiria kutwaa taji’

TIMU ya taifa ya Nigeria, Super Eagles, imerejea katika fainali za Mataifa ya Afrika baada ya kutoshiriki kwa vipindi viwili vilivyopita tangu ilipotwaa taji hilo mwaka 2013 nchini Afrika Kusini.

Sasa Super Eagles inasaka kutwaa taji hilo kwa mara ya nne. Nigeria ambayo ilimaliza kileleni katika hatua ya makundi ya kufuzu baada ya kushinda mechi nne, sare na kufungwa moja katika mechi sita imepangwa katika Kundi B pamoja na Guinea na Madagasca inayoshiriki kwa mara ya kwanza pamoja na Burundi.

Kocha Mkuu wa timu hiyo, Gernot Rohr anaamini kuwa katika mashindano ya mwaka huu hakuna kundi jepesi wakati alipozungumza na Cafonline. com kuhusu matarajio yake na mipango kwa ajili ya mashindano hayo yatakayoanza Juni 21 hadi Julai 19. Alipoulizwa kuhusu kundi lao, Rohr alisema anashukuru wamepangwa katika kundi zuri licha ya kutokuwa na nafasi ya kuchagua uwe katika zuri au baya.

Nigeria baada ya kukosa mashindano mawili baada ya kutwaa taji hilo mwaka 2013, sasa wamerejea kwa kishindo, huku ikiwa na baadhi ya wachezaji wazoefu waliocheza Kombe la Dunia 2018 nchini Russia. Nafikiri timu nyingi Afcon zin- afikiria kutwaa taji.

Tuna uzoefu kutoka katika fainali za Kombe la Dunia, lakini tulikuwa na vijana katika Kombe la Dunia, na tunafikiri bado tuna wachezaji katika Afcon. Hatuna wazoefu kama tulivyokuwa nao huko nyuma, ambako Nigeria walikuwa na wachezaji kama Austin ‘Jay-Jay Okocha, Nwankwo Kanu, au Daniel Amokachi, lakini tunatakiwa kucheza na wale tuliokuwa nao.

MKUU wa Mkoa wa Songwe, Nicodemus Mwangela ametoa siku saba ...

foto
Mwandishi: CAIRO, Misri

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi