loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Mbunge- Serikali itoe kauli homa ya dengue

MBUNGE wa Viti Maalumu, Amina Mollel (CCM) ameomba muongozo bungeni akitaka serikali itoe ufafanuzi wa hali ya ugonjwa wa homa ya dengue ambao umeendelea kuwa tishio na kuua wananchi Dar es Salaam.

Mollel ameomba muongozo huo baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali na majibu, ambapo alidai kuwa ugonjwa huo umekuwa ni tishio kwa sasa jijini Dar es Salaam huku wengi wa waliougua wakiripotiwa kufariki dunia, lakini serikali imekaa kimya.

“Mheshimiwa naomba nizungumzie tatizo lililopo jijini Dar es Salaam, hasa ugonjwa wa dengue, ugonjwa huu umekuwa tishio kwa sasa jijini humo na taarifa zilizopo ni wagonjwa wengi waliougua wamefariki dunia na hakuna taarifa rasmi ya serikali kuhusu hilo,” amesema Amina.

Amesema wagonjwa wanaokwenda hospitalini kwa ajili ya kupimwa wamekuwa wakitozwa fedha hadi Sh 50,000 na wengi wao wameshindwa kupimwa kutokana na ukosefu wa fedha.

“Naibu Spika, serikali imekuwa kimya juu ya ugonjwa huu na wanapokwenda hospitali wanaambiwa kipimo ni shilingi 50,000 kwa hiyo watu wengi wanakwepa kupima sababu ya hiyo hiyo fedha. Kwa hiyo Mheshimiwa Naibu Spika naomba ikikupendeza kutumia Kanuni ya 49 (1) (2) ili tuweze angalau tupate taarifa ama majibu kutoka kwa serikali,” amesema Amina.

Akijibu hoja hiyo, Naibu Spika Dk Tulia Ackson amesema serikali imeshatolea ufafanuzi jambo hilo kupitia taarifa zikiwemo zilizotolewa kwa vyombo vya habari.

“Waheshimiwa wabunge ugonjwa alioutaja Mheshimiwa Amina Mollel wa dengue nadhani serikali imeshatoa kauli mbalimbali katika vyombo mbalimbali.

“Kwa maana hiyo matumizi ya kanuni ya 49 mimi naweza kusema kwamba kwa sababu hii inahusu kauli za mawaziri, serikali ikiona kuna taarifa za ziada ambayo haijatoa mpaka sasa yenyewe itaomba kibali ili iweze kutoa kauli hiyo hapa bungeni kwa kutumia kanuni hiyo lakini kiti hakiwezi kutoa muongozo kwa sababu imeshatoa maelezo ya ugonjwa huo,” alisema Dk Ackson.

SERIKALI imewataka waliohujumu mali za vyama vya ushirika kujisalimisha ...

foto
Mwandishi: Ikunda Erick, Dodoma

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi