loader
Dstv Habarileo  Mobile
Taifa Stars sio timu rahisi - Kenya

Taifa Stars sio timu rahisi - Kenya

KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya Taifa ya Kenya, Harambee Stars, Sebastien Migne amesema Tanzania, Taifa Stars sio timu rahisi.

Kenya na Tanzania zipo Misri zikijiandaa kushiriki fainali za michuano ya Kombe la Mataifa Afrika, Afcon, zinazotarajiwa kuanza mwishoni mwa wiki hii. Tanzania na Kenya zimepangwa kundi C kwenye fainali hizo pamoja na Senegal na Algeria.

Akizungumza na Cafonline Migne alisema: “Senegal ni timu namba moja Afrika, Algeria pia sio rahisi, soka nchini mwao iko juu wakiwa na wachezaji wazuri… Tanzania pia itakuwa mechi nzuri, sio timu rahisi.” Tanzania imefuzu fainali hizo kwa mara ya kwanza baada ya miaka 39 na itarusha kete yake ya kwanza mwishoni mwa wiki hii dhidi ya Senegal.

“Tanzania iliifunga Uganda 3-0 kufuzu na hilo linaonesha kiwango chao, itakuwa mechi tatu nzuri na tutajaribu tuwezavyo kuweka taswira nzuri kwenye soka ya Kenya,” alisema.

“Tunahitaji kuendelea kuota, tunahitaji kuthibitisha ndoto, tuna bahati kushiriki kwenye michuano hii na tulikuwa tukihitaji.” Aidha, kocha huyo alisema, kikosi chake kipo Misri kushindana na si kuongeza idadi. Kenya ilifuzu fainali hizo baada ya kumaliza ya pili kwenye kundi G nyuma ya Ghana. Hii ni mara ya pili kwa Kenya kupangwa kundi moja na Senegal kwenye michuano hiyo. Wawili hao walikutana kwenye michuano ya mwaka 1990 na mechi iliisha kwa suluhu.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/34c06bf577355fb9af20ee054c6c7744.jpg

WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa ...

foto
Mwandishi: CAIRO, Misri

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi