loader
Ndugai atua Misri, wabunge 50 kumfuata

Ndugai atua Misri, wabunge 50 kumfuata

SPIKA wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai ametua Misri tayari kuipa hamasa timu ya Tanzania, Taifa Stars kwenye mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) yanayoanza rasmi Juni 21.

Kundi la kwanza la wabunge 50, wakiongozwa na mhamasishaji maarufu Pierre Liquid, wanatarajia kuondoka leo kuungana na Spika.

Akizungumza jana mjini hapa wakati akimkabidhi tiketi ya ndege daraja la kwanza, mhamasishaji maarufu nchini Peter Mollel maarufu Piere Liquid, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza amesema tiketi hiyo imetolewa na Waziri Mkuu ili kumwezesha Piere kwenda Misri kusaidia hamasa kwa wachezaji wa Taifa Stars.

“Wizara inaishukuru sana serikali na Waziri Mkuu kwa kutekeleza ahadi yake ya kumlipia tiketi mhamasishaji maarufu, Piere Liquid ili aende Misri kuhamasisha wachezaji wa Taifa Stars kwenye michuano ya Kombe la Afrika,” amesema Shonza.

Aliongeza kuwa Piere anaondoka leo na kundi la kwanza la wabunge 50 wanaokwenda Misri kuungana na Spika Ndugai ambaye tayari ameshafika huko kuishangilia timu ya Taifa.

Akimkabidhi tiketi hiyo, Shonza alisema Piere atakaa Misri kwa siku nne na atashuhudia mechi ya kwanza ya Taifa Stars dhidi ya Senegal, itakayochezwa Juni 23, mwaka huu.

Hata hivyo aliipongeza timu ya Taifa Stars kwa kuonesha kiwango kizuri cha mchezo kwenye mechi mbili za kirafiki ilizocheza na wenyeji Misri na kufungwa bao 1-0 na pia mechi nyingine dhidi ya Zimbabwe waliyotoka sare ya kufungana bao 1-1.

Akishukuru kwa ufadhili wa kwenda Misri, Piere alisema atahakikisha timu ya Taifa Stars inabaki kileleni katika michuano hiyo ili kuipa sifa nchi.

“Nitahakikisha nahamasisha timu yetu ibaki kileleni katika michuano hiyo, lakini pia namshukuru Waziri Mkuu aliyewezesha safari yangu kwenda Misri,” alisema Pierre.

Akizungumzia safari ya wabunge, Mwenyekiti wa Klabu ya Michezo ya Bunge, William Ngeleja alisema katika kuipa joto timu ya Taifa Stars, wabunge 83, wakiongozwa na Spika Ndugai wanakwenda Misri kuishangilia timu hiyo na tayari Spika ameshatua nchini humo.

Ngeleja alisema Bunge limetafakari na kuona umuhimu wa kuipa hamasa timu ya Tanzania hasa baada ya kupata nafasi hiyo baada ya miaka 40, hivyo wabunge hao wataenda kuishangilia ili kuipa nguvu ya kushinda.

“Tunaishukuru serikali na Bunge pamoja na kazi kubwa iliyombele yetu hivi sasa ya mkutano wa Bunge la bajeti, lakini imeonekana pia ni vyema kutaenda kuishangilia timu yetu kule Misri, na tutaenda kwa awamu mbili ili kutoa nafasi pia kwa wabunge kuchangia mjadala wa bajeti ya serikali,”alisema Ngeleja.

Alisema kundi ya kwanza la wabunge 50 wakifuatana na Piere Liquid, wanaondoka leo nchini kuelekea Misri, na Juni 21, siku ya ufunguzi wabunge hao watashuhudia mechi za ufunguzi kati ya Misri na Zimbabwe. Aidha Juni 23, watashuhudia Stars ikishuka

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/853b730943849cb24650f0cb7be7225e.jpg

SIMBA Queens imekuwa timu ya ...

foto
Mwandishi: Ikunda Erick, Dodoma

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi