loader
Michuano ya Afcon 2019 kuanza leo

Michuano ya Afcon 2019 kuanza leo

ZIKIWA zimebaki saa chache kabla ya kuanza kwa fainali za 32 za Mataifa ya Afrika (Afcon 2019) Misri, Shirikisho la Soka Afrika (Caf) limesema kuwa kila kitu kiko tayari kwa ajili ya ufunguzi rasmi.

Naibu Katibu Mkuu wa Caf anayeshughulikia Soka na Maendeleo, Anthony Baffoe alisema kuwa kila kitu kiko tayari na wanachosubiri ni kuanza kwa pambano la ufunguzi, ambalo litawakutanisha wenyeji Misri dhidi ya Zimbabwe, huku wakitarajia mashindano yenye mafanikio.

Mchezo huo utafanyika kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Cairo uliopo jijini hapa na Baffoe aliwaambia waandishi wa habari kuwa wamejipanga kwa ajili ya kuanza kwa mashindano hayo yatakayoanza Juni 21 hadi Julai 19 katika miji ya Alexandria, Cairo, Ismailia na Suez.

“Kila mmoja amejipanga kutekeleza majukumu yake vizuri ili kuyafanya kuwa mashindano bora kabisa ya Afcon, shukrani kwa Serikali ya Misri na Kamati ya Maandalizi ya Misri (LOC) kwa kazi yao nzuri waliyofanya hadi sasa, licha ya changamoto zote ya viwanja sita badala ya vinne,” alisema Anthony Baffoe.

Alisema changamoto walizokumbana nazo ni viwanja vya mazoezi kwa kila timu na kuongeza kwa kuwapatia vibali watu waliokuja na timu kutoka 30 hadi 40. Baffoe, ambaye ni mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Ghana, alisema kitendo cha kuhamishia mashindano hayo kutoka Januari-Februari hadi kuchezwa Juni-Julai, kutachangia zaidi kuongeza msisimko kwa kuwa na vipaji kibao.

Awali, wakati wa mashindano hayo baadhi ya nyota wanaocheza soka Ulaya walishindwa kushiriki baada ya kutoruhusiwa na klabu zao kutokana na mashindano hayo kufanyika sambamba na Ligi Kuu za Ulaya. “Ukiangalia Ligi Kuu ya England, wafungaji wanaoongoza kwa mabao msimu uliopita, ambao ni Waafrika watatu; Pierre- Emerick Aubamenyang (Gabon), Sadio Mane (Senegal) na Mohamed Salah (Misri), wawili kati yao wapo katika mashindano ya mwaka huu.

“Na sina uhakika kwa asilimia 100 kama Afcon ingechezwa Januari-Februari, viwango vyao vingekuwa juu kama sasa kwa sababu wangekuwa hawapo katika ligi kwa mwezi mzima.

“Haya mashindano ni makubwa na wachezaji wote nyota wa Afrika wapo hapa. Ukiangalia mechi za kufuzu viwanja vyote vilijaa hadi siku ya mchezo wa mwisho. Nilicheza wakati timu 12 zinashiriki mwaka 1992, sasa zimeongezeka mara mbili na ninaamini tutakuwa na mechi nzuri, “ aliongeza Baffoe. Akielezea kuhusu teknolojia ya mwamuzi msaidizi wa video (VAR), Baffoe alisema kuwa kwa mara ya kwanza katika historia ya Afcon, teknolojia hiyo itatumika kuanzia katika mechi za robo fainali.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/9b1d21a95d4a3c630f94c5f830a4aa74.jpg

WAFANYABISHARA mbalimbali wa Temeke, ...

foto
Mwandishi: CAIRO, Misri

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi