loader
Dstv Habarileo  Mobile
Kocha- Kugomea bonasi kumeongeza ari

Kocha- Kugomea bonasi kumeongeza ari

KOCHA Mkuu wa timu ya taifa ya Cameroon, Clarence Seedorf anasema mabingwa hao wa Afrika wako vizuri na hawajaathirika na sakata la bonasi ambalo lilichelewesha safari yao ya kwenda Misri kwa ajili ya fainali za Mataifa ya Afrika, Afcon 2019.

Cameroon leo wataanza kampeni zao za kutetea taji hilo kwa kucheza dhidi ya Guinea-Bissau lakini walitua hapa Cairo Ijumaa baada ya kugoma kuondoka nchi mwao hadi sakata za bonasi klimetatukliwa.

Wachezaji wa Simba hao wa wasiofungika walikataa ofa ya dola za Marekani 34,570 kwa ajili ya kushiriki, na walikubali kupanda ndege baada ya kuzungumza na viongozi wa michezo wa nchi hiyo.

Kulikuwa na wasiwasi kuwa huenda sakata hilo lingepunguza au kumaliza matumaini ya timu hiyo kutwaa taji hilo kwa mara ya sita, lakini Seedorf aliliambia kundi la vyombo vya habari vya Cameroon juzi kuwa wachezaji hawajaathirika kabisa na suala hilo.

“Tuko vizuri na timu ina utulivu wa kutosha na tunajua nini kilichotuleta hapa. Hakuna muda ambao ari ya timu ilibadilika. Tuna kundi lenye furaha, na kila mchezaji anajua jukumu lake na umuhimu wa mashindano hayo,” amesema Seedorf.

“Ukweli sakata lile la bonasi ndio kwanza limeiongezea nguvu timu na kuwa na nia ya kufanya vizuri. Kuna kama kawasiwasi lakini wachezaji wameonesha ukomavu na wameamua kuwa hapa na kuipigania Cameroon.

“Sakata la bonasi sio kitu kukifikiria hasa kwa Cameroon au Afrika, nimeona matukio yanayofanana dunia nzima lakini sitaki hilo liharibu lengo letu. Camaroon wanaanza kampeni zao za kutetea taji bila ya nyota wake Vincent Aboubakar na Jean Pierre Nsame, wote wako nje ya mashindano haya kutokana na maumivu.

Licha ya wachezaji 10 tu waliokuwa katika Afcon ya Gabon 2017 na kutwaa ubingwa, kocha huyo Mholanzi anaamini mashabiki wengi wanatumaini kuiona timu yao kucheza fainali ya nne mwaka huu.

“Cameroon ni timu ya pili kutwaa mataji mengi ya Afcon baada ya wenyeji Misri waliotwaa mara saba na kama mabingwa watetezi wanatarajia kuona kitu fulani kizuri kutoka kwa Simba hao.

“Tunatakiwa kucheza na kuonesha uwajani kwanini sisi tunapewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingswa. Nafikiri nina vipaji vya kutosha na uwezekano wa kufanya kitu muhimu sana katika mashindano haya. Seedorf pia alitupilia mbali madai kuwa na wachezaji wasio na uzoefu, katika kikosi cha wacheaji 11 katika Kombe la Mataifa ya Afrika kwa mara ya kwanza, kunaweza kuikosesha nafasi timu hiyo kufanya vizuri.

“Natumaini huo utakuwa msukumo kwa wachezaji wapya lakini pia tuna wachezaji wenye uzoefu katika kikosi chetu, ambao walishinda la mashindano hayo, hivyo kuna uwiano mzuri.”

“Kwa kweli hakuna timu dhaifu katika mashindani haya, na mpambano huo ulikuwa mgumu dhidi ya Zimbabwe. Wakati wote tunataka kuwa wa kwanza na kufanya vizuri kuongoza kundi.”

Cameroon itaanza kampeni zake za kuwania taji hilo la 2019 dhidi ya Guinea-Bissau Juni 25 katika Kundi F kabla ya kucheza na Ghana Juni 29. Mabingwa watetezi hao wa Afrika watamaliza kampeni zake kwa kucheza dhidi ya Benin Julai 2.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/712fdfc1f58d559bfe35787a4865e0e7.jpg

Kiungo mshambuliaji wa Brazil, Neymar JR amesema Kombe ...

foto
Mwandishi: CAIRO, Misri

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi