loader
Makonda kuipokea Stars kesho

Makonda kuipokea Stars kesho

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kesho atakuwa miongoni mwa wadau wa michezo watakaojitokeza kuipokea timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, iliyoshiriki michuano ya 32 ya Kombe la Mataifa ya Afrika, Afcon 2019, Misri itakaporejea nchini.

Makonda kupitia ukurasa wake wa Instagram amethibitisha kuwa atakuwepo katika Kiwanja cha Kimataifa cha Ndege cha Julius Nyerere (JNIA) kuwapokea wachezaji wa timu hiyo watakapokuwa wakirejea.

Stars imetolewa hatua hiyo baada ya kupoteza michezo yote mitatu dhidi ya Algeria 3-0, Kenya 3-2 na Senegal 2-0 na kutoka mikono mitupu bila ya pointi hata moja na kushindwa kuifikia rekodi ya mwaka 1980 iliposhiriki kwa mara ya kwanza na kuondoka na pointi moja. Makonda ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Hamasa ya kikosi hicho, aliandika ujumbe kuhusu Stars kupitia ukurasa wake wa kijamii wa Instagram kuwa atawapokea na kuwapongeza kwa kuitangaza nchi.

“Nawapenda na nitawapokea kesho kutwa yaani (kesho) kwa sababu nyingi sana ila moja kubwa mmeonesha tungeweza kushinda na ndio maana makosa yameonekana hata kwa wale wasiojua mpira,” alisema. Aliendelea kufafanua kuwa Stars inaweza kuwa timu kubwa hapo baadaye iwapo kama wataanza maandalizi ya Afcon kwa msimu wa 2021 mapema.

“Hongereni sana Taifa Stars mmeitangaza nchi iwe kwa kufungwa au kutoka raundi ya kwanza. Kupitia nyie watu wameijua Tanzania,” aliandika Makonda. Baada ya kikosi hicho kurejea kitapumzika kidogo kisha kitaanza maandalizi ya michuano ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN). Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Muddy Mkangala alisema mjini Cairo, Misri jana kuwa, timu hiyo ilitarajia kuondoka Misri saa nane na dakika 20 usiku wa Julai 3 na ndege ya Ethiopian Airline.

Wachezaji hao jana walialikwa nyumbani kwa Balozi wa Tanzania nchini Misri, baada ya hapo timu moja kwa moja itaenda kiwanja cha ndege tayari kwa safari hiyo. Stars inatarajiwa kucheza mchezo wa kwanza dhidi ya Sudan Julai 26, mwaka huu Dar es Salaam kisha watarudiana Agosti 2, mwaka huu nchini Sudan kwa ajili ya kusaka nafasi ya kufuzu kwa fainali za CHAN.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/16b75d68efecce35777c01128c1c3367.jpg

ZAIDI ya Vijana 25,000 kutoka ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi