loader
Bocco- Kahata ataniongezea mabao

Bocco- Kahata ataniongezea mabao

USAJILI wa kiungo Francis Kahata, kwenye klabu ya Simba, umemfurahisha nahodha wa timu hiyo John Bocco, ambaye amefunguka akieleza namna kasi yake ya ufungaji itakavyoongezeka.

Alhamisi iliyopita Kahata kiungo bora wa misimu miwili iliyopita kwenye Ligi Kuu ya Kenya, alisaini mkataba wa miaka miwili ya kuwatumikia mabingwa hao wa Tanzania Bara, ambao wamepania kufanya makubwa zaidi msimu ujao.

Akizungumza na gazeti hili, Bocco alisema anatambua uwezo aliokuwa nao Kahata, na kusema ana uhakika idadi ya mabao ya kufunga itaongezeka ukilinganisha na ile ya msimu uliopita alipomaliza nafasi ya nne akifunga mabao 16.

“Sina shaka na uwezo wake, nimekuwa nikimfuatilia kwa karibu hata tulivyokuwa Misri kwenye michuano ya Afcon, kutua kwake Simba naamini kutaisaidia timu yetu pamoja na sisi washambuliaji katika mbio za ufungaji,” alisema Bocco.

Nahodha huyo pia alizungumzia usajili unaoendelea kufanywa na timu yake, ambapo alisema unampa matumaini ya kubeba ubingwa wa Afrika baada ya msimu uliopita timu hiyo kutolewa na TP Mazembe katika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Alisema anatambua kwamba ushindani wa nafasi ya kucheza utakuwa mkubwa, lakini hilo litasaidia kuifikisha timu yao katika mafanikio makubwa.

Washambuliaji wengine waliopo kwenye kikosi cha Simba ni mfungaji bora wa msimu uliopita Meddie Kagere, Deo Kanda kutoka TP Mazembe na Mbrazili Wilker Henrique da

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/1f8d17c3e3bdfbd87d0575a63d580ac7.jpg

TAASISI ya Mama Ongea ...

foto
Mwandishi: MOHAMED AKIDA

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi