loader
Dstv Habarileo  Mobile
Spika ashinda kesi ya kumpinga

Spika ashinda kesi ya kumpinga

SPIKA wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA), Dk Martin Ngoga ameibuka kidedea katika rufaa iliyowasilishwa na Burundi, kupinga kuchaguliwa kwake.

Rufaa hiyo iliwasilishwa katika Mahakama ya Afrika Mashariki (EACJ) jijini Arusha.

Katika hukumu yake iliyotolewa mwishoni mwa wiki iliyopita, mahakama hiyo ilitupilia mbali rufaa hiyo, ikieleza kuwa imekosa vielelezo muhimu na ushahidi wa kutosha kuwa spika huyo hakuchaguliwa kihalali kushika wadhifa huo.

Moja ya vielelezo muhimu ambavyo serikali ya Burundi ilipaswa kuwasilisha mahakamani kama ushahidi ni orodha ya mahudhurio ya wabunge, waliopiga kura siku hiyo ili kuonesha namna uchaguzi ulivyokwenda hadi mshindi kupatikana.

Kwa mujibu wa EACJ, kielelezo hicho na nyaraka nyingine muhimu, zilitosha kumtia hatiani spika huyo anayetokea nchini Rwanda.

Kutokana na kukosekana kwa nyaraka hizo, mahakama iliamua kuitupa rufani hiyo na kuhalalisha uchaguzi uliompitisha Dk Ngoga kama Spika wa Bunge la Afrika Mashariki.

Kiongozi wa majaji wa mahakama ya EACJ, Jaji Monica Mugenyi alisema kigezo kilichowasilishwa na Nestor Kayobera ambaye ni Mbunge wa EALA kutoka Burundi, kilikuwa ni uchaguzi wa spika sio halali, kwa sababu wakati wa uchaguzi huo kuna wabunge walikosekana.

“Ni wazi kuwa wabunge wote wa EALA ni watu wazima na walishuhudia tukio lote la uchaguzi hadi mshindi kutangazwa. Hoja ya Mheshimiwa Nestor Kayobera kuwa hata yeye mwenyewe hakuwepo wakati wa uchaguzi huo hakufanyi matokeo kuwa sio halali,” alisema Kayobera.

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi