loader
Dstv Habarileo  Mobile
Inter Milan yamtolea macho Lukaku

Inter Milan yamtolea macho Lukaku

BOSI wa Inter, Antonio Conte amesema Romelu Lukaku atakiimarisha kikosi chake, lakini amekiri kwamba kuna mambo ya kusimamia kama unataka kumsajili mshambuliaji kutoka Manchester United.

Inter imekuwa ikimuwania Mbelgiji huyo lakini haijakutana bado na United kumzungumzia mchezaji huyo aliyewagharimu pauni milioni 75 kumsajili kutoka Everton miaka miwili iliyopita.

“Unajua nampenda huyu mchezaji,” alisema Conte. “Siku za nyuma nilipokuwa kocha wa Chelsea [mwaka 2016 mpaka 2018] nilijaribu kumleta Chelsea.”

“Kama nilivyosema, nampenda mchezaji huyu na namchukulia kama mchezaji muhimu kwetu kufanya vizuri lakini kama ilivyo, kuna soko la usajili.”

“Tunajua vizuri hali yetu ilivyo kwa sasa tutaona cha kufanya, lakini kwa sasa Lukaku ni mchezaji wa United.”

Kitendo cha Inter kumtaka Lukaku kimezua maswali mengi kuhusu hatima ya Mauro Icardi, ambaye hajasafiri na klabu yake katika maandalizi ya msimu Asia na kuzidisha tetesi ya kwamba anataka kuondoka.

Alipoulizwa kuhusu mshambuliaji huyo wa Argentina, Conte alijibu “Mazingira yako wazi klabu iko wazi kwamba Icardi hayupo kwenye mpango wa Inter, huo ndio ukweli.”

Akijibu kuhusu hatima ya Lukaku United, kocha Ole Gunnar Solskjaer alisema hakuna taarifa zaidi. Lukaku amekosa mechi zote za ziara ya timu yake Australia kutokana na kuwa majeruhi na Solskjaer alisema anabaki kuwa hayupo. “Hayuko fiti, hatopatikana,” alisema bosi huyo wa United.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/1552a6657dcc6b3d85b10fc936fe1a2d.jpg

BAADA ya Yanga kuondolewa kwenye michuano ya Ligi ...

foto
Mwandishi: MILAN, Italia

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi