loader
Picha

Costech ina jukumu la kuchambua bunifu zinazouzika

MKURUGENZI Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia, Dk. Amos Nungu amesema hivi sasa wamejipanga kutoa elimu vyuoni ya kuwajengea uwezo wanafunzi kwa kuanzisha kumbi za ubunifu ili waelewe ni bunifu gani zinaweza kuleta majibu chanya kwa watanzania.

Dk. Nungu alisema hayo leo ikiwa ni siku ya mwisho ya kufungwa kwa maonyesho ya 14 ya Elimu ya Juu ambayo yamefanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Alisema lengo la kuwajengea uwezo ni kuwawezesha wabunifu mbalimbali kubuni vitu ambavyo vinatokana na changamoto mbalimbali katika jamii na vinavyoweza kupatiwa majibu chanya yatakayosaidia.

“Kazi kubwa tunajenga uwezo kwa kumbi za ubunifu. Kuna bunifu ambazo mbunifu kaangalia changamoto na kutengeneza majibu yake. Tuna jukumu kubwa la kuchambua bunifu zinazouzika,” alisema.

Alisema katika suala la ubunifu Costech ipo tayari kufanya kazi na kila mtu ili kuhakikisha wabunifu wanasaidika.

Alisema katika kipindi hiki cha kuelekea uchumi wa viwanda, Costech inataka kuwafikia wabunifu huko waliko kwa kutoa elimu.

CHAMA cha Wanasheria Tanganyika (TLS) wamewasilisha mapendekezo kwenye Kamati ya ...

foto
Mwandishi: Lucy Ngowi

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi