loader
Picha

Wachimbaji wauza dhahabu ya mil 25/-

WACHIMBAJI wadogo wa dhahabu katika mgodi mpya wa Ndurutu, Kijiji cha Kilama Kata ya Iyogwe wilayani Gairo, mkoa wa Morogoro wamepata neema kwani hadi Juni 30, mwaka huu.

Jumla ya gramu 255. 23 za dhahabu zilinunuliwa katika soko la madini la Morogoro mjini na kupatikana jumla ya Sh milioni 25.3 na Serikali ikiwa imekusanya tozo zinazofi kia kiasi cha Sh milioni 1.8.

Kaimu Ofisa Madini Mkazi wa mkoa wa Morogoro , Emmanuel Shija alisema hayo kuhusu hatua mbalimbali zilizochukuliwa katika mgodi mpya wa dhahabu wa Kilama uliogunduliwa na wachimbaji wadogo wa eneo la kitongoji cha Mlimani kipindi cha mwishoni mwa mwezi Mei mwaka 2019.

Shija alisema tangu uchimbaji umeanza chini ya utaratibu na usimamizi uliowekwa katika eneo hilo, hadi kufikia Juni 30, 2019 gramu 228.3 za dhahabu zilinunuliwa na madalali wa eneo la Kilama , ambapo wanunuzi wa dhahabu watano wamesajiliwa na mgodi huo na kupewa leseni kwa mujibu wa sheria.

“Jumla ya gramu 255.23 za dhahabu kutoka mgodi wa Kilama zimenunuliwa katika soko la Madini lililopo Morogoro mjini na dhahabu hizo zimenunuliwa kwa jumla ya Sh 25, 341, 725 . 27 na Serikali imekusanya tozo zake zinazofikia jumla ya Sh 1,849,945 .94,” alisema Shija alipozungumza na gazeti hili. Hata hivyo, alisema leseni nne za utafiti na uchimbaji mdogo wa madini (PML) zimeombwa na Ushirika ulioundwa chini ya utaratibu unaosimamiwa na halmashauri za wilaya ya Gairo.

Pamoja na hayo, alitoa rai kwa uongozi wa ushirika ambao umekabidhiwa kuongoza mgodi huo wafanye kazi ya usimamizi kwa weledi na uaminifu ili kuhakikisha wachimbaji wadogo wanafanya kazi wananufaika na mgodi huo lakini pia na serikali inapata stahiki zake zilizo kwa mujibu wa Sheria.

Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Siriel Mchembe kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Kebwe Stephen Kebwe aliufungua tena mgodi huo Julai 7, mwaka huu baada ya kufungwa Juni 8, mwaka huu kutokana na wachimbaji watano kufariki dunia kwa kufukiwa na miamba ya mawe na kujeruhiwa pia.

Hata hivyo, kufunguliwa kwa mgodi huo kumekuja baada ya wachimbaji wadogo kutimiza masharti yaliyotolewa na Dk Kebwe juu ya kuweka mazingira mzuri ya uchimbaji, kuunda vikundi vya ushirika vya wachimbaji na kusajiliwa na halmashauri ambapo jumla ya vikundi 97 vilikuwa vimesajiliwa.

RIPOTI ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za ...

foto
Mwandishi: John Nditi, Morogoro

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi