loader
Picha

Ajib aahidi raha Simba

BAADA ya ukimya wa muda mrefu kwa mchezaji Ibrahimu Ajibu kurejea kwenye kikosi cha Simba akitokea kwa mahasimu wao Yanga, amevunja ukimya na kudai amendoka kwa amani bila kinyongo na mtu yeyote.

Alisema amefanya hivyo kwa kujua wazi kazi yake ni kucheza mpira kuna leo na kesho mambo yakiharibika iwe rahisi kwake kurudi tena kwa miamba hao waliomfanya ang’are vilivyo msimu uliopita.

Nyota huyo kwenye msimu ulipita wa Ligi Kuu Tanzania Bara alitoa mchango mkubwa kwenye kikosi cha Yanga , mbapo alisaidia mara 17 na kupachika mabao saba kiasi cha kumfanya aliyekuwa mshambuliaji Heritier Makambo kufunga mabao mengi.

Ajibu amesema amejiandaa vizuri kukabiliana na upinzani wa kupigania namba kwenye kikosi hicho kuhakikisha anawakonga nyoyo mashabiki wa timu hiyo wanaonekana kufurahishwa na ujio wake huo baada ya kuwa nje ya kikosi hicho kwa miaka miwili.

“Nimejiandaa vizuri kulinda kiwango changu na kuhakikisha natengeneza nafasi na kutoa pasi za mwisho kama nilizokuwa natoa nikiwa Yanga, Nawaomba mashabiki wa Simba wasiwe na wasiwasi mambo mazuri yanakuja, “amesema Ajibu.

KUELEKEA mchezo wa Ligi Kuu England utakaochezwa Jumapili kati ya ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi