loader
Picha

Wanafunzi Filbert Bayi mabingwa Umisseta

SHULE za Filber Bayi zimewapongeza wanariadha waliotwaa ubingwa wa jumla katika Michezo ya 40 ya Shule za Sekondari Tanzania (Umisseta) iliyofanyika mkoani Mtwara mwaka huu.

Katika hafla hiyo ya chakula cha mchana iliyofanyika katika ukumbi wa shule hizo uliopo Mkuza, Kibaha, wanariadha hao walitwaa medali 14 za dhahabu, mbili za fedha na mbili za shaba, walipongezwa na kukabidhiwa vyeti.

Mkurugenzi Mkuu wa shule hizo, Anna Bayi alisema kuwa wanafunzi hao ambao wanasomeshwa bure katika shule hiyo, wamefanya jambo kubwa katika mkoa wa Pwani kwa kuuwezesha kushika nafasi ya kwanza katika riadha, licha ya uongozi wa mkoa kukaa kimya.

Aliwapongeza vijana hao kwa matokeo mazuri ya Umisseta na kusisitiza kuwa siri ya mafanikio na maandalizi mazuri licha ya changamoto zilizokuwepo za wilaya kushindwa kufuata utaratibu wa kuwachukua wanafunzi kuwapeleaka katika mashindano ya mkoa.

Alisema baada ya mafanikio ya Kibiti, timu nzima iliyoundwa na wanariadha wengi wa Filbert Bayi ilichaguliwa kuunda timu ya mkoa na kwenda kushindana Mtwara katika Michezo ya Umisseta Taifa, ambako nako walishinda.

Filbert Bayi pekee katika mashindano hayo ya taifa walitwaa medali 18, kitu ambacho sio kidogo na ndio maana waliamua kuwapongeza kwa hafla hiyo, ambayo inawafanya watoto kujiona kuwa wanatambulika.

Alisema mbali na kung’ara katika michezo, Bayi alisema pia kuwa wachezaji hao ni tishi pia katika taaluma na sio kweli kuwa wachezaji hawana uwezo michezoni, kinachotakiwa ni kupanga ratiba nzuri ya masomo na michezo.

Alisema kuwa hakuna mtu asiye na uwezo ila kinachotakiwa ni juhudi na malengo ya kufanya vizuri katika michezo mbalimbali. Aliwataka viongozi wa mikoa kuwapongeza watoto wengine walioshiriki michezo ya Umisseta ili kuwatia moyo hata kama hawajarudi na medali, kikubwa ni kuwapokea na kuwapa pole kwa kushiriki na kufanya vizuri katika michezo hiyo.

Alisema mwakani watawafanyia sherehe wachezaji wa michezo yote watakaoshiriki Umisseta kutoka mkoa wa Pwani hata kama uongozi wa mkoa hauko tayari kufanya hivyo.

Wanariadha wa shule za Filbert Bayi waliotwaa medali ni Regina Mpigachai aliyepata medali tatu za dhahabu na moja ya shaba, huku Gaudencia Maneno akitwaa medali tatu za dhahabu, huku Benedicto Mathias alitwaa medali mbili za dhahabu na moja ya fedha.

Wakati Helemengilda Nkulilei alipata medali mbili za dhahabu na moja ya shaba wakati Pili Mipawa alipata medali mbili za dhahabu, Amos Charles alipata medali moja ya dhahabu na moja ya fedha huku Esther Martin alitwaa medali moja ya dhahabu.

Pia katika hafla hiyo alikuwepo mwanafunzi wa shule ya Kibaha Moses Chacha aliyepata meali ya dhahabu, ambaye naye alikabidhiwa cheti cha shukrani kama wengine wa Filbert Bayi.

Mkurugenzi wa shule hizo, Bayi alisema kuwa watoto hao wako katika program maalum ya kusoma bure kutokana na vipaji vyao vya riadha na tayari wameshapata wanariadha watano watakaowasomesha bure shuleni hapo kuanzia kidato cha kwanza kuanzia mwakani.

TIMU ya Taifa ya soka ya wanawake chini ya umri ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Kibaha

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi