loader
Picha

Mhasibu atuhumiwa kuiba mil 84/- za jiji

MHASIBU wa Halmashauri ya Jiji la Arusha, Charles Jacob anasakwa na mwajiri wake na ametakiwa kujisalimisha Kituo cha Polisi kabla ya kumpiga pingu kwa madai ya kutafuna Sh milioni 84 fedha za makusanyo ya kila mwezi kuanzia Machi, mwaka huu katika mzani wa mazao ya chakula.

Akizungumza na vyombo vya habari baada ya kutembelea mizani ya mazao iliyopo kwa Mrombo, jijini Arusha, Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Dk Maulid Madeni amesema tangu mizani hiyo ilipoanzishwa Machi, mwaha huu imekuwa ikiingiza Sh milioni 2.8 kwa siku lakini mhasibu huyo amekuwa akiwasilisha kwenye akaunti ya halmashauri Sh 110,000 tu kwa siku huku fedha nyingine zikiishia mfukoni mwake.

Mhasibu huyo pamoja na wasimamizi wa mizani hiyo,Thobias Julius na Agness Loishiye ambao wanashikiliwa polisi, wanadaiwa kusababisha upotevu huo wa fedha na kuisababishia hasara kubwa halmashauri hiyo.

Dk Madeni aliwakamata na kuwaweka ndani wafanyakazi hao na kuagiza Jacob ambaye hakuwepo kazini kujisalimisha mwenyewe Kituo cha Polisi na kwamba hadi sasa hapatikani nyumbani kwake hata simu yake ya mkononi haipatikani.

Kwa mujibu wa Dk Madeni, kituo hicho cha kukusanya ushuru hakifanyi vyema na kusababisha fedha nyingi kuishia mikononi mwa wakusanyaji na mhasibu huyo.

Awali, wafanyakazi hao walipewa nafasi ya kujitetea na kufafanua kuwa wameshindwa kukusanya mapato kutokana na magari kuwa machache, hawafahamu kama fedha wanayokusanya kama inafika au haifiki katika halmashauri.

Mchumi wa Jiji la Arusha, Anna Mwambene amesema wamekuwa wakifuatilia vyanzo vya mapato kuangalia utendaji wa kazi, kubaini upotevu wa fedha unaofanywa na watendaji wasio waaminifu.

NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na ...

foto
Mwandishi: John Mhala, Arusha

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi