loader
Picha

Magufuli kufungua Mkutano Mkuu ALAT

RAIS John Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa mkutano mkuu wa 35 wa Jumuiya ya Tawala za Mikoa Tanzania (ALAT). Mkutano huo wa siku tatu utafanyika jijini Mwanza kuanzia leo hadi Julai 24.

Akizungumza na gazeti hili jana, Katibu Mkuu wa ALAT Taifa, Elirehema Kaaya alisema pamoja na mambo mengine, mkutano huo utakuwa na ajenda ya msingi ya kujadili utendaji wa jumuiya hiyo na miradi mbalimbali ya maendeleo inayosimamiwa na halmashauri nchini.

“Rais wetu amekuwa kinara na msimamizi mkuu wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini, kwa kutambua hilo tumeona tumpe heshima ya kufungua mkutano huu muhimu,” alisema.

Alisema maandalizi ya mkutano huo ambao umetanguliwa na vikao vya kamati ya utendaji yameshakamilika na kwamba utahudhuriwa na wakurugenzi watendaji, wenyeviti wa halmashauri, miji na majiji 185 na wabunge 26 kutoka mikoa yote nchini.

Kaaya alisema wananchi wa mkoa wa Mwanza watanufaika kiuchumi na mkutano huo.

“Mkutano huu pamoja na washiriki wake, jumla unatarajia kuwa na washiriki karibu 400, hawa si wachache ni wengi, hivyo ni matumaini yetu kuwa wakazi wa jiji la Mwanza wataitumia vizuri fursa hii kujieletea maendeleo,” alisema Kaaya.

CHAMA cha Wanasheria Tanganyika (TLS) wamewasilisha mapendekezo kwenye Kamati ya ...

foto
Mwandishi: Nashon Kennedy, Mwanza

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi