loader
Picha

JPM atoa maagizo kwa Simbachawene, Bashe

Rais John Magufuli amemuagiza Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira, George Simbachawene aondoe vikwazo katika utoaji vibali vya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) ili kuongeza kasi ya uwekezaji.

Rais ametoa agizo hilo leo Ikulu, Dar es Salaam baada ya kumuapisha Simbachawene kuchukua nafasi ya January Makamba ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Magufuli pia leo amemuapisha Hussein Bashe kuwa Naibu Waziri wa Kilimo.

Dk Magufuli amesema, wawekezaji wamekuwa wakicheleweshwa kuwekeza nchini kwa sababu kutopata vibali.

"Sisi tunataka kuwa na viwanda vya kutosha na wawekezaji wasiwekewe vipingamizi kwa visingizo vya NEMC kwa sababu tunahitaji viwanda ikiwezekana wawekeze viwanda, vibali vya NEMC vitakuja baadaye" amesema Rais Magufuli.

Rais pia amemtaka Simbachawene asimamie suala la Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na awe chachu ya Muungano huo kwa kuhakikisha anashirikiana na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan katika utekelezaji wa majukumu yake.

Amesema, amemteua Bashe kwa sababu michango yake bungeni hivyo sasa akaitekeleze kwa vitendo.

“Nimekuwa nakusikiliza bungeni, michango yako imekuwa mizuri ,unatoa analysis namna kilimo kinaweza kuleta production kikaleta effect katika uchumi wetu…sasa zile zilikuwa za bungeni nataka ukazifanye kwa practical (kwa vitendo)... ukayafanye kweli kweli" amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli jana alimteua Simbachawene, na pia akamteua Bashe kuchukua nafasi iliyokuwa imeachwa wazi na Innocent Bashungwa ambaye hivi karibuni aliteuliwa kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara.

CHAMA cha Wanasheria Tanganyika (TLS) wamewasilisha mapendekezo kwenye Kamati ya ...

foto
Mwandishi: Ombeni Utembele

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi