loader
Picha

Bashe aanza kazi, wakulima kusajiliwa

Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe ameanza kazi kwa kuhudhuria kikao kazi cha uongozi wa juu wa wizara hiyo kuelezwa taswira na mwelekeo wa mamlaka hiyo ya Serikali.

Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga ameongoza kikao hicho katika ofisi ndogo za wizara hiyo jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri wa Kilimo Omary Mgumba na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mhandisi Mathew Mtigumwe wamehudhuria kikao hicho.

Waziri Hasunga amewataka wasaidizi wake wafanye kazi kwa bidii na kwa kushirikiana ili kutimiza azma ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Magufuli ya kuimarisha uchumi kupitia viwanda.

Hasunga ametoa taswira ya muelekeo wa wizara hiyo kwa mipango ya muda mfupi na muda mrefu kwa kuzingatia weledi na utendaji uliotukuka kwenye utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2015/2020.

Miongni mwa mambo aliyobainisha Hasunga ni pamoja na umuhimu wa kuanzishwa Sheria ya Kilimo itakayotoa suluhisho la changamoto zinazamkabili mkulima na sekta ya kilimo kwa ujumla.

“Kuna kila sababu ya kuanzishwa haraka sheria ya kilimo na tayari tupo katika hatua za mwisho, kwa sababu hatuna Sheria ya Kilimo na inayotumika sasa ni Sera ya Kilimo iliyotungwa mwaka 2013 ambayo pia inahitaji kupitiwa upya” amesema

Amesema, sheria inayotumika sasa ni ya Bodi za Mazao Mbalimbali, ambayo pia inachangamoto zake na kuna mazao ambayo hayana bodi hivyo ni vigumu kuwatetea wakulima wa mazao hayo.

Mazao yaliyo katika utaratibu wa bodi ni pamoja na pamba, kahawa, chai, korosho, pareto na tumbaku, na mazao ya chakula hayana bodi lakini yana mchango mkubwa katika uchumi wa Taifa.

Hasunga pia ameeleza kuhusu usajili wa wakulima wa mazao yote na kwamba, bodi za mazao ziliagizwa kuwapa wakulima vitambulisho ili kuwatambua  iwe rahisi kuwahudumia.

Pia ameeleza umuhimu wa Wizara ya Kilimo kuanzisha Bima ya Mazao kwa kuwa kwa muda mrefu wakulima nchini wamekosa utetezi wanapopata na majanga yakwemo ya uchache wa mvua.

Muda mfupi kabla ya kikao hicho Rais Magufuli alimuapisha Bashe kuwa Naibu Waziri wa Kilimo kuchukua nafasi ya Innocent Bashungwa ambaye hivi karibuni aliteuliwa kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara.

CHAMA cha Wanasheria Tanganyika (TLS) wamewasilisha mapendekezo kwenye Kamati ya ...

foto
Mwandishi: Mathias Canal, Wizara ya Kilimo

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi