loader
Picha

January atoa neno la mwisho

Aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba amemshukuru Rais John Magufuli kwa kumuamini na kumpa jukumu la kuiongoza wizara hiyo.

Rais Magufuli jana alitengua uteuzi huo na akamteua George Simbachawene kuiongoza wizara hiyo.

Simbachawene ameapishwa leo Ikulu, Dar es Salaam.

Katika hafla hiyo, Rais Magufuli pia amemuapisha Hussein Bashe kuwa Naibu Waziri wa Kilimo.

Kwenye ukurasa wake katika mtandao wa kijamii wa twitter Makamba ameandika; “Neno la Mwisho kwenye hili: Namshukuru Rais kwa kuniamini, Makamu wa Rais kwa kunielekeza, PM kwa kunisimamia, na Team ya VPO /NEMC na Mawaziri wote kwa ushirikiano.”

VPO ni Ofisi ya Makamu wa Rais, na NEMC ni Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira.

“Nampongeza @HusseinBashe na Simbachawene kwa kuaminiwa. Nawatakia heri na kuwaahidi ushirikiano wangu wa dhati.”ameandika Makamba.

Jana baada ya Rais Magufuli kutengua uteuzi wa Makamba, kijana huyo aliandika kwenye ukurasa wake huo; “Kwa kweli nimeyapokea mabadiliko yaliyofanywa kwa moyo mweupe kabisa kabisa . Nitasema zaidi siku zijazo.”

CHAMA cha Wanasheria Tanganyika (TLS) wamewasilisha mapendekezo kwenye Kamati ya ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi