loader
Picha

Simbachawene atekeleza ‘hapa kazi tu’

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira George Simbachawene ameanza kutekeleza majukumu yake kwa kuzungumza na kiongozi wake, Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan kwenye ofisi ndogo ya Makamu wa Rais, Dar es Salaam.

Simbachawene aliteuliwa jana kuiongoza Wizara hiyo kuchukua nafasi ya January Makamba, na ameapishwa leo Ikulu jijini humo.

Baada ya kuapishwa Simbachawene alikwenda ofisini akakaribishwa na Naibu wake Mussa Sima, na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Joseph Malongo.

Simbachawene ni Mbunge wa Kibakwe mkoani Dodoma na hadi alipoteuliwa alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti.

Baada ya Rais Magufuli kumuapisha Simbachawene aliumuagiza aondoe vikwazo katika utoaji vibali vya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) ili kuongeza kasi ya uwekezaji.

Dk Magufuli amesema, wawekezaji wamekuwa wakicheleweshwa kuwekeza nchini kwa sababu kutopata vibali.

"Sisi tunataka kuwa na viwanda vya kutosha na wawekezaji wasiwekewe vipingamizi kwa visingizo vya NEMC kwa sababu tunahitaji viwanda ikiwezekana wawekeze viwanda, vibali vya NEMC vitakuja baadaye" amesema.

Rais pia amemtaka Simbachawene asimamie suala la Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na awe chachu ya Muungano huo kwa kuhakikisha anashirikiana na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan katika utekelezaji wa majukumu yake.

CHAMA cha Wanasheria Tanganyika (TLS) wamewasilisha mapendekezo kwenye Kamati ya ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi